NA CHAUSIKU SAIDA _MATUKIODAIMA_APP MWANZA.
Wafanyabiashara wa soko la Kirumba Jijini Mwanza waliohamia Magomeni ili kupisha ujenzi wametakiwa kufanya biashara zao kwa amani na utulivu huku wakisubiri kukamilika kwa soko Hilo.
Hayo yamebainishwa na Diwani wa kata ya kirumba Wessa Juma wakati akifanya mahujiano na waandishi wa habari na kueleza kuwa mbali na changamoto mbalimbali zilizopo katika katika soko jipya walilohamia wanapaswa kuwa wavumilivu.
Juma Alisema kuwa anawapongeza wafanyabiashara waliohama kwa hiari yao wenyewe ili kupisha ujenzi wa soko la kisasa litakalokuwa na miundombinu rafiki kwa watu wote wenye ulemavu na wasio na ulemavu.
"Nimefurahi kuona wafanyabiashara wa soko la kirumba wamehamia soko la magomeni kwa hiari yao mwenyewe hawajalazimishwa na mtu yeyote ili kupisha kuanza kwa ujenzi wa soko la kisasa katika eneo hilo" Alisema Juma.
Aidha ameishuru serikali ya awamu ya 6 kwa uamuzi wake wa kujenga soko la kisasa katika eneo hilo litakalo gharimu zaidi ya bilioni 17 ikiwa ni pamoja na ujenzi wa miundombinu ya barabara kuzunguka sehemu hiyo.
“Naipongeza serikali ya awamu ya sita kwa dhamira yao ya kutaka kuanza kujenga eneo la soko letu la Kirumba kwa muundo wa kisasa huku barabara kuzunguka eneo hilo urefu wa kilomita 2.9 zitajengwa kwa mawe” alisema Wesa.
Naye Mwenyekiti wa wafanyabiashara Soko la Kirumba Elias Daud alisema kuwa wafanyabiashara wenyewe wametengeneza maeneo ya kuuzia bidhaa zao wenyewe na kuhama eneo hilo kuanzia siku ya Jumamosi.
Alisema zaidi ya meza 400 na maduka zaidi ya 100 zimeandaliwa katika eneo hilo huku akiomba halmashauri ya Manispaa ya Ilemela kutengeneza miundombinu kwa ajili ya maji taka ya wauza samaki, kuku vilevile kujengwa kwa mtaro wa maji na kusogezwa kwa huduma ya umeme
0 Comments