Na Matukio daima media , Mbarali
KUELEKEA maadhimisho ya siku ya wazee duniani baraza la wazee wilayani Mbarali mkoani Mbeya limewaomba vijana kuwapunguzia mzigo wa kulea wajukuu bila sababu za msingi hali inayopelekea wazee hao kuelemewa na mzigo wa kulea licha ya vijana kuwa na nguvu za kutosha .
Hayo yamesemwa jana na Katibu Msaidizi wa Baraza la wazee wilayani humo ,Christina Mwalyaje wakati akizungumza na mtandao huu jinsi walivyojipanga kuelekea maadhimisho ya siku ya wazee duniani ambayo hufanyika tarehe 1/10/2022 kila mwaka kama sehemu ya kuleta usawa na kuboresha maisha ya wazee.
Mwalyaje alisema kuwa kwa wilaya ya mbarali maadhimisho hayo yamepangwa kufanyika kwa ngazi ya katika kata ya Igurusi ambapo ujumbe wa maadhimisho hayo ni “Ustahimilivu na mchango wa wazee ni muhimu kwa maendeleo ya Taifa”.
“Umri wetu sisi wazee tumechoka sana lakini sasa tunatwishwa mzigo mkubwa wa kulea wajukuu na ukiangalia wengine hatuna nguvu tena za kuhangaika na wajukuu hivyo tunaomba vijana watupunguzie mzigo kwani kwa umri huu tulionao tunahitaji kupumzika na sio kuhangaika tena “alisema Mwalyaje.
Hata hivyo Katibu huyo aliwaomba viongozi wa dini kusherekea sikukuu hiyo muhimu pamoja na wazee kwa kuendelea kuwaombea wazee wote afya njema,kufanya ibada maalum kwa ajili ya wazee wa Taifa ndani ya nyumba za ibada pamoja na kuelimisha waumini juu ya uzee na maandalizi ya uzee na kuzeeka.
Mwalyaje alisema kuwa faraja nyingine ambayo wanapaswa kupatiwa wazee ni misaada ya chakula, nguo,dawa na mahitaji mengine muhimu kwa wazee wanaoishi katika hali ya umaskini uliokithiri.
Alisema kuwa kitu kingine wanachopaswa kuwasaidia wazee ni kuomba waumini wa dini mbali mbali kuendelea kuwasaidia wazee wanaoishi pekee yao katika umaskini mkubwa na wazee wengine wenye uhitaji .
“Lakini tunawaomba waumini Kuwakumbusha kuwalinda wazee wanawake dhidi ya mila na desturi zilizopitwa na wakati,wazee wanapaswa kulindwa ,kulelewa na kutetewa dhidi ya vitendo vya ukatili pamoja na kuwaonyesha upendo na faraja”alisema.
Akizungumzia kuhusu miundo mbinu ya kwenye nyumba za ibada Katibu Mwalyaje alisema nyumbza za ibada zote ziendelee kujenga miundo mbinu rafiki kwa wazee walemavu ili waweze kushiriki ibada vizuri.
Meneja miradi wa Shirika lisilokuwa la kiserikali linalojishughulisha na masualaya wazee wilayani Mbarali (KIWWAUTA),Moses Nchimbi alisema wanashirikiana na mabaraza ya wazee na Halmashauri ya wilaya ya mbarali katika kufanya maadhimisho hayto ya wazee kwa ngazio ya kata kuanzia septemba 21 kwa tarehe tofauti m paka October mosi mwaka huu siku ya kilele.
“Kazi kubwa ambayo pia tumekuwa tukifanya ni kuhamasisha wazee kuendelea kupata chanjo ya Covid-19 kupitia mabaraza yao ya vijiji ambayo yapo katikla maeneo mbali mbali bado tunawapatia wazee elimu ya kujinga na Covid 19 kama inavyoelekezwa na wizara ya Afya na na shirika la afya duniani (WHO)”alisema.
Hata hivyo Nchimbi alisema kuwa shirika hilo limekuwa mstari wa mbele katika kusaidia wazee wilayani humo pamoja na kusimamia masuala mbali mbali ya kwenye jamii ambayo yanakuwa yanawakabili .
0 Comments