Header Ads Widget

ZAIDI YA MILIONI 45 KUTUMIKA KUFUATILIA MIRADI YA AFYA MANISPAA YA LINDI.

 


NA HADIJA OMARY, MATUKIO DAIMAAPP,LINDI

ZAIDI ya shilingi milioni 45 zinatarajiwa kutumika kwenye utekelezaji wa mradi wa ufuatiliaji wa matumizi ya fedha katika rasilimali za Umma katika miradi ya Afya inayotekelezwa katika kata tatu za Manispaa ya Lindi Mkoani humu.



 

Mradi huo wa Kuimarisha Uwezo wa Ufuatiliaji wa Rasilimali za Umma kwa Jamii katika  Sekta ya Afya Halmashauri ya Manispaa ya Lindi ’unatekelezwa na shirika lisilo la kiserikali linalojulikana kama shirika la  usaidizi wa kisheria Mingoyo (SHIMKIMI)  kwa ufadhiri wa foundation for civil society (FCS).



 

 Akizungumza wakati wa ghafla ya utambulishaji wa mradi  kwa watendaji   ngazi ya kata zitakazonufaika na mradi huo na viongozi wa ngazi ya manispaa na Wilaya, katika ukumbi wa Mikutano wa DDC Mjini Lindi mapema leo September 22, 2022  Ofisa wa Mradi huo Mohamedi Paris  alisema lengo kubwa la kufuatilia miradi hiyo  ni kuongeza uwajibikaji kwa jamii ili kuongeza ubora wa bidhaa na huduma kwenye sekta ya Afya.



 

Alisema mradi huo utatekelezwa katika  mitaa sita kwenye kata tatu za manispaa ya Lindi ambazo ni Kata ya Mnazi mmoja katika mtaa ya Zahanati na Ruhaa, kata ya Ng’apa katika mtaa wa Cheleweni na Mahakamani na kata ya Chikonji katika Mtaa wa Nanjing a na koleni.

 


“Utekelezwaji wa miradi hii ya Ufuatiliaji wa Rasilimali za Umma kwa Jamii katika  Sekta ya Afya ni moja ya utekelezaji wa sera namba tano ya Afya ambayo  inaeleza juu ya uwajibikaji wa kijamii (social accountability) ambapo foundation for civil society (FCS) ni wadau muhimu katika hili ndio maana hata sisi tupo hapa tunashiriki” alieleza Paris



 

Kwa upande wake mchumi wa manispaa ya Lindi, Mwandishi Nchimbi amesema mradi huo utakuwa na manufaa kwa jamii kwa sababu unalenga kuangalia namna rasilimali za Serikali zinavyotumika katika taasisi za umma.


 

“ manufaa ya mradi huu yatakuja kuonekana kwa jamii baada ya kuona huduma za Afya zitakapokuwa zimeboreka kwa sababu nao wakigundua kama wanafuatiliwa itawasukuma kuendelea kutoa huduma kwa usahuhi na kwa makini zaidi”


Naye Afisa Mtendaji wa Kata ya Mnazi mmoja Geoge Komba alisema kwa kuwa mradi huo unakwenda kuonyesha uwajibikaji wa kila mmoja katika majukumu yake ili kuleta uwazi  na kuongeza tija kwenye uwajibikaji viongozi wa Serikali katika maeneo husika wanao wajibu wa kutoa ushirikiano kwa Shirika hilo.

 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI