NA MATUKIO DAIMAAPP,MTWARA
Mkuu wa Wilaya ya Masasi Claudia Kitta amewataka wakulima wa zao la Muhogo Wilayani humo kuhakikisha wanazalisha muhogo wenye ubora utakao waongezea soko ndani na nje ya nchi,
Akizungumza katika mafunzo yaliyoandaliwa na Shirika la Ubora wa Viwango nchini (TBS) alisema kuwa wakulima wa muhogo wamekuwa wakilima na kuongeza thamani zao hilo ambapo mafunzo hayo yataenda kuwaboresha zaidi.
Alisema kuwa muhogo huo wenye viwango utakaoweza kuongeza thamani ya bidhaa hiyo sokoni wakulima wanapaswa kuongeza uzalishaji kwakulima mashamba makubwa.
“Wakulima walime muhogo kwa wingi soko kwa ndani bado hatujatosheleza bado soko la ndani lipo kubwa muhogo ni zao zuri mkulima akilima kwa tija na kuvuna mazao yenye ubora na akajua namna bora ya kuvuna na kusindika tunaamini kuwa litamnyanyua mkulima” alisema Kitta
Nae Meneja Utafiti na mafunzo kutoka TBS Hamis Sudi alisema kuwa mafunzo hayo yanalenga kuongeza thamani ya biashara zao la muhogo nchini.
Katika mafunzo haya tunawewsezesha kuongeza tija katika shughuli zao za kiuchumi kwenye mazao ya Muhogo, Viungo na Mpunga ambapo kwa mikoa ya lindi na mtwara tuupa muhogo kipaumbele kwakuwa ni moja kati ya zao ambalo linalimwa kwa wingi”
“Tunataka bidhaa zenye viwango zinazokubalika kaitka soko la ndani na nje kwa kuwaelimisha kanuni bora za kilimo taratibu zake utunzaji uvunaji na kuangalia kiafya na namna bora ya usindikaji wa bidhaa hizo katika ufungashaji na kuangalia afya na usalama wa watu unazingatiwa” alisema Sudi
Afisa Kilimo Wilaya ya Masasi Andrea Kalinga alisema kuwa wakulima wamekuwa na mwitikio mkubwa wa kulima zao hilo.
Alisema kuwa mwitikio huo pia umekuwa mkubwa kwkuwa hata mbegu wanapatiwa na shirika la la meda hivyo kuwapa nafasi wakulima kuongeza uzalishaji ambapo ili kuongeza thamani TBS wametoa mafunzo ya ubora ili kupata bidhaa yenye ubora.
Mpaka sasa tunao wakulima 378 wanaolima zao la muhogo na mengine mchanganyiko ambapo kwa sasa wale wakulima waliokuwa wakilima hekali moja au mbili lakini kwa sasa wameongeza wanalima hekali tano.
Kwa mafunzo haya tuliyopata hapa tunaamin kuw atutaongeza msoko mazuri zaidi kwakuwa tutakuwa tumezalisha muhogo wenye tija zaidi wenye viwango viwanavyotakiwa kitaifa na kimataifa” alisema Kalinga
0 Comments