Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma
RAIS Samia Suluhu Hassan amewataka watafiti wa lishe kuhakikisha wanafanya Utafiti wa masuala ya lishe ili kukabiliana na tatizo ya kukosa nguvu ya kiume kwa vijana na wanaume kwa ujumla .
Alisema vijana wengi hapa nchini wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya kukosa nguvu za kiume na kukimbilia kula mavitu yasioyofaa yote inatokana na lishe duni.
Rais Samia ameyasema hayo leo Septemba 30, 2022 wakati wa hafla ya utiaji saini mkataba wa usimamiaji shughuli za lishe jijini Dodoma.
"Kama watafiti wetu hawatafanya tafiti na kubaini tatizo hasa nini niwazi kwamba matatizo haya hayatapatiwa ufumbuzi niwazi kwamba tutakuwa na Taifa lenye vijana gaigoi ambao ndio tunawategemea nguvu Kazi ya Taifa," alisema Rais Samia.
"Watafiti twendeni tukafanye Kazi ili tuwaokoe vijana wetu walio kwenye balehe kuhangaika kunywa supu ya pweza au udongo wa kongo (VUMBI LA KONGO)," alisema Rais Samia.
Kwa Upande wake Waziri wa Afya Ummy Mwalimu Alisema mkataba huo wa usimamiaji wa shughuli za lishe
Utakwenda kusaidia Masuala ya lishe kwani lishe mbovu imekuwa ikichochea Magonjwa ya mara kwa mara.
Alisema lishe Bora ni msingi wa Maendeleo ya mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla .
Naye waziri kutoka Ofisi ya RaisTawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Innocent Bashugwa alimshukurua Rais Samia kwa kuwapatia Shilingi bilioni 160 kwa ajili ya madarasa 8000.
Alisema fedha hizo zitakwenda kukamilisha Madarasa hayo 8000 ambayo ndio yaliokuwa yamepelea .
Hata Hivyo Rais Samia akizundua magari 52 ambayo yatakwenda kwa Maafisa elimu katika kuhakikisha wanaboresha Masuala ya elimu pia akizundua pikipiki 517 ambazo zinakwenda kuboresha huduma za Afya.
0 Comments