Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma
KATIBU wa Halmashauri Kuu wa Itikadi na Uenezi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Shaka Hamdu Shaka amesema zaidi ya wagombea Milioni 2 wamejitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya Chama hicho kuku akikili kwamba idadi hiyo ya wagombea haijawai kutokea katika chaguzi zote zinazofanyika .
Pia alisema kutokana na muitikio Mkubwa kwa wanachama wanaotaka kugombea nafasi mbalimbali muda wa kuchukua fomu umeongezwa kwa upande wa nafasi wa Halmashauri Kuu ya Taifa Chama cha mapinduzi nafasi 15 Zanzibar na nafasi 15 Tanzania Bara na nafasi za mikoani Tanzania bara na Zanzibar waweza kukamilisha zoezi hilo kwa kila mwenye nia
Hayo aliyasema leo September 27 Jijini Dodoma Wakati akiongea na waandishi wa Habari mara baada ya kumalizika kwa kikao Cha Halmashauri Kuu ya CCM kilichoketi Jijini hapa chini ya Mwenyekiti wa wa CCM Taifa Samia Suluhu Hassan huku akisema mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi kwa nafasi mbalimbali ndani ya Chama kuanzia ngazi ya Shina Tawi Kata na kwa upande wa Zanzibar ngazi ya Jimbo uchaguzi unefanyika vizuri na kwa mafanikio na kwasasa ni uchaguzi ngazi ya wilaya.
Alisema Kila baada ya Miaka mitano kwa mujibu ya ibara ya 82 kifungua kidogo cha kwanza ya Chama cha kinaekekeza kila baada ya Miaka mitano kufanyika uchaguzi wa kuwachagua viongozi ngazi ya wilaya, wakiwemo wenyeviti wa Wilaya kwa upande wa Chama cha mapinduzi lakini na jumuiya wa Chama cha mapinduzi sambamba na Viongozi wanapokwenda kuungana na Viongozi wengine ndani ya chama na
"Niseme wazi tangu kuanza kwa mchakato wa uchaguzi ngazi ya shina hadi leo Wilaya zoezi zima limefanyika kwa ufanisi na mafanikio makubwa licha ya changamoto za hapa na pale ," alisema Shaka.
Aidha kuanzia tarehe 22 mwezi huu hadi leo September 27 kulikuwa na vikao vya kitaifa kwa Maana ya Sekretarieti Halmashauri Taifa, Kamati Kuu ya Halmashauri ya Taifa Kuu ya Taifa ,Halmashauri Kuu ya Chama cha mapinduzi taifa , Kamati maalumu ya Halmashauri kwa Upande wa Zazibar vikao vyote vimefanyika kwa mujibu ya kalenda na vilikuwa vikao maalumu.
Pia alisema Halmashauri Kuu pamoja na Mambo mengine kimefanya uteuzi wa mwisho kwa kufanya uteuzi wa mwisho kwa nafasi ya wagombea uwenyekiti wa ngazi wa Wilaya nchi nzima katika Wilaya 168 kwa Wilaya za kichama .
"Tumeshapata wagombea ambao watakwenda kusimama kwenye uchaguzi wa ngazi ya wilaya kuanzia tarehe 1 hadi 2 Octoba 2022 nchi nzima," alisema .
"Niwatake Sasa kila mwenye sifa ya kuwachagua kufika siku hiyo ili kuweza kuwachagua kwani hadi Sasa maandalizi yameshakamilika ,"alisema Shaka
Hata hivyo alisema Halmashauri Kuu ya Chama cha mapinduzi CCM inatoa rai uchaguzi ufanyike kwa haki na maadili ya ungozi vitendo vya rushwa visitokee na chaguzi hizo zikamilike kwa muda uliopangwa.
Mwisho






0 Comments