Header Ads Widget

ALIYEKUWA MEYA WA MOSHI JUMA RAIBU ACHANGIA UJENZI OFISI YA KATA

 


Na Gift Mongi,Matukio DaimaAPP,Moshi

Aliyekuwa meya wa Manispaa ya Moshi Juma Raibu, ametoa vifaa vya ujenzi kwa ajili ya kukamilisha jengo la ofisi ya kata ya Kaloleni iliyopo manspaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro.


 Akizungumza leo jumanne 26,2022 diwani huyo wa kata ya boma mbuzi, amesema katibu wa chama CCM taifa,Daniel Chongolo alitoa bati sabini, wakati wa ziara yake katika manispaa hiyo na kwamba na yeye ameamua kutoa mbao zenye thamini ya zaidi ya sh 2 milioni kwa ajili ya kupaua jengo hilo pamoja na choo.


Amesema kukamilika kwa ujenzi wa jengo hilo kutarahisisha makatibu wa chama kukaa ofisini na kufanya kazi za kusikiliza wananchi pamoja na kutatua kero zao kwa kuwa CCM ndio chama kinachoisimamia serikali.


"Kazi za ya chama ni kusimamia kusimamia maendeleo ya wananchi, na kama chama hakina ofisi maendeleo ya wananchi yatakuwa hafifu hivyo nimeamua kuchangia ili kukamilisha ujenzi wa ofisi hiyo wananchi wapate maendeleo".  Amesema Juma


Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi kata ya kaloleni Mrisho Mgambo, amewaomba wadau mbalimbali kujitokeza kwa ajili ya kukamilisha ujenzi huo.


Amesema hadi kukamilika kwa ujenzi huo zaidi ya sh13milion zitatumika na kwamba hadi sasa sh3milioni milioni zimetumika.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI