Na Fatma Ally Matukio Daima APP Dar es Salaam
Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imesema inaendelea kufanya vizuri kutokana na makusanyo yao ya ndani ambapo inajipanga kila mwaka kuongeza fedha za mapato yao ya ndani kwa ajili ya kuboresha huduma za jamii.
Kauli hiyo imetolewa Leo jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji Mhandisi Amani Mafuru wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kusoma na kupitisha taarifa za hesabu za Serikali za mwisho wa mwaka.
Amesema kuwa, mwaka uliopita makusanyo ya ndani yalikua madogo ikilinganishwa na mwaka huu ambapo yameongezeka, huku akielezea fedha zinazokusanywa za mapato ya ndani na zinazotoka Serikali kuu zinakwenda katika miradi ya maendeleo ikiwemo shule, vituo vya afya pamoja na masoko.
Aidha, amesema kuwa ni takwa la kisheria hesabu za Halmashauri ziwe zinamfikia mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali baada ya miezi mitatu ya mwaka wa fedha kumalizika, ambapo
baada ya taarifa hizo kupitiwa Halmashauri imewasilisha taarifa ya hesabu za mwisho katika kikao cha baraza la
madiwani.
"Sisi Halmashauri vya Jiji la Dar es Salaam tulikamilisha hesabu hizo na zikapitiwa na kamati ya ukaguzi jana tulikuwa na kikao cha kamati ya fedha ,utawala taarifa hizo zikawasilishwa katika kamati ya fedha na utawala ambao inajumuisha baadhi ya Madiwani ambao wanawakilisha wenzao " amesema Mhandisi Mafuru.
Ameongeza "Madiwani wameipokea na kupitia kadili walivyoona inafaa wamepitisha ili iweze kuwasilishwa kwa Mshibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali kwa muda uliopangwa kwa maana ya septemba 30 tunashukuru waheshimiwa madiwani wameipokea na wameipitisha na wameiridhia iweze kufikishwa kwa CAG" amesema Mhandisi Mafuru.










0 Comments