NA THABIT MADAI, ZANZIBAR
MSHAURI wa Benki ya Dunia katika Masuala ya Kilimo na Ufugaji Ephraim Masako ametoa Wito kwa Wakulima Nchini kulima kwa kufuata Kanuni na Utaratibu za Kilimo huku wakizingatia Matumizi sahihi ya Ardhi.
Pia amewataka, kujenga utaratibu wa kutembelea Miradi mikubwa mikubwa ya Kilimo kwa lengo la kujifunza namna ambavyo wawekezaji katika Sekta hiyo walivyofanikiwa.
Wito huo ameutoa wakati akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kutembele Miradi wa Kilimo cha Vanila na Vitunguu swaumu pamoja Ufugaji wa Njiwa kwa Utalii katika Kijiji cha Uwekezaji huko Bungi Mkoa wa Kusini Unguja ambapo amesema hatua hiyo itasaidia kuwakuza Wakulima wadogo wadogo na kuwa wakulima wakubwa huku wakinufaika na mazao mbalimbali.
Amesema, Wakulima wanapaswa kuwa na Matumizi sahihi ya Ardhi ambapo wanawezaa kulima mazao tofauti tofauti katika eneo moja na kunufaika.
Amesema katika Nchi zilizofanikiwa Wakulima Wadogo huwa wanajifunza kupitia wakulima wanaondesha Miradi vmikubwa ili kujifunza na kukuza Kilimo chao.
“Ili Wakulima Wetu waweze kufanikiwa wanapaswa kujifunza kwa wale waliofanikiwa katika Miradi mikubwa ya Kilimo na Kujifunza mbinu bora za Kilimo,”amesema.
Akizungumzia ziara yake hiyo ameeleza namna alivyofurahishwa kutokana na Uwekezaji Mkubwa katika Kilimo cha Vanila na Ufugaji wa Njiwa wa Kisasa kwa Utalii.
“Tokea nifike katika eneo hili nmejifunza mambo mengi ikiwemo matumizi mazuri ya ardhi na nimefurahishwa na mwekezaji hapa alivyoweza kutumia eneo dogo kulima kilimo cha zaidi ya zao moja,” amefafanua.
Amefafanua kuwa, Mwekezaji katika eneo la Vanila anaendesha kilimo hicho kwa Uwazi huku akiwataka wananchi kujitokeza kuwekeza katika Kilimo hicho.
“Niwapongeze Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kumpatia eneo mwekezaji huyu kwa kuendesha Kilimo na Ufugaji ni vyema sasa Wananchi kujitokeza ili kuumuunga mkono katika Kilimo chake,”asema.
Kwa Upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Vanila Village Simon Mkodya ameeleza kufurahishwa kwa kupokea ugeni huo Mshauri kutoka Benki ya Duniani na kueleza kuwa matumaini yake kutegemea makubwa kutoka kwake.
“Leo nimefurahishwa kupokea mgeni huyu ambapo naamini atakuwa mwakilishi mzuri wa kuelezea kile ambacho amejifunza kutoka katika Vanila na mazao mengine yaliyopo Shambani hapo,”ameeleza.
Mradi wa Vanila umetoa ajira zaidi ya 270 kwa vijana Visiwani Zanzibar ambao unatekelezwa na Vanila International Limited.
0 Comments