NA HAMIDA RAMADHAN, DODOMA
SERIKALI imeombwa kuchukua muda wa haraka kutathimini ubunifu mbalimbali zinazobuniwa na wanafunzi wa vyuo ili kuziendeleza na kuweza kutoa ajira kwa vijana wengi wakitanzania kwa lengo la kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.
Ombi hilo limeombwa na Mwanaafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Elizabeth Massawe ambaye amebuni mashine ya 'Automatic Milk Vending' ambayo inatumia mfumo wa kidigitali kuuza maziwa na kumrahisishia mfanyabiashara kupunguza gharama za kuajiri na badala yake atakuwa anangalia kwa kutumia mfumo huo kujua wateja wangapi walionunua maziwa na amepata kiasi gani kwa siku
Akizungumza leo na Matukio Daima Blog , kwenye maonesho ya maadhimisho ya Siku ya wahandisi jijini hapo katika banda la NIT, Elizabeth alisema kuwa mashine hiyo inafanya kazi kwa kutumia mfumo wa kidigitali ambapo mfanyabiashara atakaa nyumbani huku biashara yake ya maziwa inaendelea kama kawaida.
Mwanafunzi huyo ameeleza kuwa mteja atakapohitaji maziwa ataweka kiasi cha fedha na atapata maziwa kulingana na hela yake huku akitolea mfano mteja huyo akiweka shilingi 100 atapata maziwa milimita 300 na taarifa itamfikia mmiliki kupitia web site yake.
Alisema lengo la kubuni teknolojia hiyo ili kumsaidia mfanyabiashara asitumie mikono na muda mwingi kufanya biashara hiyo kama kusafisha kila dakika katika eneo lake la biashara na ukusanyaji wa hela.
"Mmiliki wa hii mashine atakuwa anajaza maziwa pale yatakapokuwa yameisha na kuendelea na shughuli nyingine na atajua kupitia mfumo wateja wangapi wamenuna maziwa na kiwango cha fedha kinaonekana, tarehe na muda wa mteja alionunua maziwa," alisema mwanafunzi huyo.
Amefafanua kuwa kupitia mashine hiyo mmiliki atajua ameuza kiasi gani na wateja wangapi waliofika kununua maziwa na glasi ngapi kwa siku ameuza.
Elizabeth alisema hadi kukamilika kutengeneza mashine hiyo imechukua muda wa miezi miwili na gharama za malighafi ni shilingi 180,000.
Akizungumzia changamoto katika utengeneza wa mashine hiyo Elizabeth amesema kuungua kwa vifaa mara kwa mara hali iliyomsababishia kufikisha muda huo.
Kwa upande wake Mkufunzi Uhandisi wa Matengenezo ya ndege kutoka NIT, Castory Njako amesema kuwa miongo mwa bunifu zilizofanya vizuri chuoni hapo na baadae zikashindanishwa wakati wa maonesho ya Siku ya wahandisi wanawake bunifu hizo zilishinda.
Aidha amewakaribisha wananchi wa Dodoma kwenda kuona fani za uhandisi mbalimbali zinazotolewa na chuo hicho huku akiwahamasisha vijana kujiunga.
Mwisho
0 Comments