Header Ads Widget

MBUNGE PROF. PATRICK NDAKIDEMI ATAKA SHULE ZOTE ZA SERIKALI ZINAPATA HATI MILIKI.

 


NA WILLIUM PAUL.

Mbunge wa Jimbo la Moshi Vijijini Prof Patrick Ndakidemi alihoji Serikali inamikakati gani kuhakikisha kwamba shule zote za kata na za Serikali kwa ujumla zinapata hati miliki.


Mbunge huyo aliuliza swali hilo jana katika mkutano wa Bunge unaoendelea jijini Dodoma.



Akijibu swali hilo kwa niaba ya Waziri wa  OR-TAMISEMI Naibu Waziri David Silinde amesema kuwa Serikali ipo katika mpango huo na wamehamasisha Halmashauri zote kutekeleza Jambo hili.

"Lengo la Serikali kwa sasa ni kuhakikisha shule zote zinakuwa na hati miliki na tumeshazielekeza halmashauri zote nchi kuanza kulifanyia kazi jambo hili" alisema Naibu Waziri Silinde.

Mwisho..

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI