Na Matukio DaimaAPP, Mtwara
Timu ya wasichana wa wa kijiji cha Mnyembe imefungwa gori sita na Timu ya Wasichana ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania Kituo cha Naliendele katika mechi ya kirafiki ilivyochezwa kituoni hapo.
Akizungumza mara baada ya kumaliza mchezo huo Captain Timu Tari Jamila Ndovu alisema kuwa hakuna timu ya kuweza kuwafunga ndani ya mkoa huo kwakuwa wamejiandaa.
Alisema kuwa wamekuwa wakifanya mazoezi na pia wanakocha mzuri ambaye wanaamini kuwa ataweza kuwafikisha mbali.
“Kikosi chetu kilikuwa kizuri ndio maana tumeshinda tunaomba kuwahamsishsa watoto wa kike wajitokeze tucheze nao ila wakumbuke kwa uwanja wa nyumbani hatoki mtu lazima akae”
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Dr Furtunus Kapinga alisema kuwa wamekuwa wakitumia michezo kutoa elimu juu ya tafiti zinazofanyika katika taasisi hiyo.
“Kabla hawajacheza tuliwatembeza ili kuona kazi mbalimbali tunazofanya ili waweze kupata elimu nini wanapaswa kufanya ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha uwekezaj kwenye mazao mbalibali ikiwemo mbogamboga na matunda”
“Mechi hii ya kilafiki tumecheza nao na tunaamini tutaendelea kushirikiana nao michezo inajenga mahusiano na kutoa elimu juu ya tafiti mbalibali tunazofanya hapa kiutoni” alisema Dr Kapinga
Nae Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mtwara Mikindani Shadida Ndile alisema kuwa wasichana hao wamechagua michezo bora yenye hamasa kubwa duniani.
“Nimefurahi kuona wasichana wakiungana na kutengeneza timu ya mpira wa miguu hii inaonyesha wazi kuwa wametambua kuwa michezo ni ajira kupitia timu hizi nimeweka mikakati ili kuweza kupata timu ya mkoa wetu kwa wasichana” alisema Ndile
MWISHO
0 Comments