Header Ads Widget

CRDB WAJA NA KAMPENI YA TISHA NA TEMBO KADI

 



Benki ya CRDB kanda ya kusini imezindua kampeni ya tisha na Tembo Card itakayowezesha wateja kupata shilingi  milioni 3 pamoja na safari ya kwenda kuangalia  kombe la dunia Qatar.


Akizindua kampeni hiyo Meneja Majengo na Huduma za Ndani za Benki ya CRDB Kanda ya Kusini Leevan Maro alisema wamezindua ili kuwezesha wateja kupata zawadi mbalimbali ikiwemo safari ya kwenda Qatar. 


“tumezindua huduma hii ili wateja wetu waweze kuchanja kwakutumia tembo card  ambapo ndani ya miezi mitatu hakutakuwa na tozo na washindi watachukua shilingi milioni 3 pamoja na safari ya kwenda kuangalia kombe la dunia kwa wateja wakubwa wanne watakao chanja sana katika kamepeni hiyo”



Nae Meneja mahusiano kwa wateja  wa benki hiyo Salma Suleima alisema kuwa kampeni hiyo itawahusu wateja wote hivyo ni vema wanwake wakijitokeza kwa wingi zaidi. 


“Wanawake wengi ni wafanyabishara niwahimize wafungue akaunti katika benki yetu ili waweze kuushiriki katika kampeni hii muhimu kwa wateja ili waweze kupata fursa ya kuangalia kombe la dunia  Qatar”


Kwa upande wake meneja mwandamizi wa kitengo cha kadi kutoka benk ya CRDB Karingiton Chahe alisema kuwa watanzania jitokezeni kwa wingi kufungua akati katika benki yetu. 


Itawapa fursa ya kulipia kwakutumia kadi kwa kuchanja tu bila kutembea na fedha mfukoni wakati huohuo itatuweka katika kampeni ambayo wisho wa siku tutashinda kwenda kuangalia kombe la dunia ama pesa shilingi milioni 3”






MWISHO

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI