Wakazi wa jiji la Tanga wanatarajia kuongeza maeneo ya kuburudika kwa tamasha la chomachoma festival litakalozinduliwa Leo September 10,2022 katika viwanja vya Mwahako jijini Tanga
Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Halmashauri la jiji la Tanga,Mwnyekiti wa chama cha chomachoma festival,Elizabeth Chawenda alisema tamasha hilo litakuwa likifanyika mara mbili mwezi
Alisema kwamba kwenye tamasha hilo kutakuwa na aina zote za Nyama ikiwemo ya ngo'mbe,mbuzi ,kuku na samaki
Chawenga alisema Tamasha hilo litakuwa linafanyika kila juma most na juma pili ya mwezi kuanzia asubuhi mpaka usiku kwa lengo kuwapatia fiursa wakazi wa Tanga ya kupumzika baada ya kazi za wiki nzima
Hata hivyo,Chawenda alifafanua kuwa kutakuwepo na burudani mbali mbali ikiwemo ngoma mziki mnene na michezo kwa watoto
Alisema kutakuwa na vinywaji vingi na vya aina zote ikiwa ni pamoja na vinywaji laini na vikali
"Nawaomba wakazi wa Tanga wafike kwa uwingi wao ili kufanikisha shughuli hiyo ya aina yake"alisema Chawenda ambae pia ni Meneja wa NMB Bank Mkoani Tanga
Pia alitoa wito kwa wakazi wa Wilaya za jirani ikiwemo Muheza,Mkinga na Panga I kujitokeza kwa wingi kuja kujumuika na wakazi wa jiji la Tanga katika starehe hii isiyo na kiingilio
Tamasha hilo la aina yake linatarajiwa kuzinduliwa na mgeni rasmi ambae ni Mkuu wa Wilaya ya Tanga,Hashim Mgandilwa katika viwanja vya maonyesho ya biashara Mwahako jijini Tanga
Tanga choma choma Festival limedhaminiwa na taasisi ya SIDO,SELF Micro Finance,Tanga jiji na wenyeji NMB ambae ndie mratibu wakuu wa Tanga choma choma Festival.
0 Comments