NA MATUKIO DAIMAAPP
Afisa Muhifadhi wa Shirika la Uhifadhi wa Mazingira Duniani (WWF) Deogratius Kilasara asemsema kuwa shirika hilo limekuja na mbinu ya kuwadhibiti tembo kwenda kwenye makazi ya watu kwakuwafunga kifaa maalum ‘colla’.
Kauli hiyo ameitoa wakiwa katika kikao na wakurugenzi maafisa maliasili TAWA, TANAPA na PAC ambapo alisema kuwa wamekuja na mpango mkakati wa ili kusaidia wananchi ambao wanaumizwa na kuharibiwa makazi na mashamba yao na wanyama wakali na waharibifu.
“Tumeona malalamiko ni mengi kutoka kwa wananchi hivyo tukaamua kuchukua jitihada za makusudi kwa kushirikiana na Wizara na TAWILI pamoja na TAWA ili kuona namna gani sahihi ya kudhibiti wanyama hao”
“Zoezi la kuwafunga vifaa maalum (collas) vitawezesha kuwafatilia na kugundua mienendo yao wakiwa ndani na nje ya hifadhi ambapo itatupa nafasi ya kuweza kuwafatilia kwa ukaribu”
“Kazi yetu kubwa ni uhifadhi wa mazingira ndani ya jamii tumekuwa na wanyama wakali na waharibifu hususani tembo ambaye amekuwa akifanya uharibifu kwa kusababisha kifo na kuharibu mazao”
“Baada ya serikali kuanzisha hivi vituo ambavyo vitajengwa katika halmashauri zenu maneo mbambali tukao na tukutane na tujadili namna gani vitaendeshwa ili viweze kuwa na tija kwa jamii” alisema kilasara
Nae Kamanda wa Uhifadhi Kanda ya Kusini Mashariki TAWA Abraham Jullu alisema kuwa Serikali inatarajia kujenga vituo 16 nchi nzima lakiini kwa kanda hii watajenga vituo vitano vitakavyuo gharimu zaidi ya shilingi milioni 400.
“Tunayokazi kubwa tuliyopangiwa kufanya ikiwemo kulinda mapori tengefu, viwanja vya ndege na tutafungua vituo hivi vitano mwezi wa kumi kanda ya kusini mashariki”
“Hivi vituo vinaenda kuwa shirikishi kwa maana ya askari wa wanyamapori kutoa msaada kwa jamii wanapovamiwa na wanyama wakali na waharibifu kutokana na uchache wao tutashirkiiana na jamii husika” alisema Jullu
0 Comments