Header Ads Widget

MIUNDOMBINU UMEME WA GRIDI YA TAIFA KIGOMA YAHUJUMIWA

 


Na Fadhili Abdallah,Kigoma

 

WATU wasiojulikana wamefanya hujuma kwenye miundo mbinu ya shirika la uzalishaji na ugavi wa umeme nchini (TANESCO) inayosafirisha umeme wa gridi  ya Taifa kutoka kituo cha Nyakanazi wilaya ya Biharamulo mkoa Kagera kupeleka umeme huo mkoa Kigoma na hivyo kufanya wilaya nne za mkoa Kigoma zinazotoa njia hiyo kukosa umeme.



Meneja wa TANESCO mkoa Kigoma, Mhandisi Jafari Mpina akitoa taarifa kwa waandishi wa habari mjini Kigoma leo mchana alisema kuwa tukio hilo limetokea kwenye kijiji cha Itumbiko wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma usiku wa kuamkia leo.



Katika hujuma hiyo Mhandisi Mpina alisema kuwa watu hao wamechoma moja ya nguzo zinazosafirisha umeme huo, kung’oa vyuma kwenye baadhi ya nguzo hizo na kisha kuandika mabango kwamba umeme usipopelekwa eneo la kijiji cha Itumbuko  hujuma hizo hazitaisha na umeme huo hautaenda kwenye hizo wilaya nyingine.



Kutokana na kuhujuma kwa nguzo hizo meneja huyo wa TANESCO mkoa Kigoma alisema kuwa wamelazimika kuzima umeme huo tangu alfajiri ya leo na matengenezo kwa ajili ya kuweka miundo mbinu mingine imeanza na kwamba walitarajia huduma hiyo kurejea tena leo jioni.


Moja ya nguzo za umeme ambayo imechomwa moto katika tukio la   hujuma ya miundo mbinu ya umeme wa gridi lililofqnywa kijiji cha Itumbiko wilaya ya Kakonko mkoa Kigoma


Wilaya zilizoathirika na hujuma hiyo ni wilaya ya Kakonko, Kibondo na Buhigwe ambazo ziliungwa kwenye gridi ya Taifa wiki moja iliyopita baada ya kuzimwa kwa mashine za kuzalisha umeme zinazotumia mafuta.


“Tayari suala hili limesharipotiwa polisi na hatua za uchunguzi wa suala hilo limeanza lakini mafundi wanaendelea na matengenezo kuhakikisha huduma zinarudi leo,”Meneja wa TANESCO Kigoma alisema hayo  akizungumza na waandishi wa habari.


Bango lenye ujumbe ambalo limeandikwa na watu hao kueleza sababu ya  kuharibu miundo mbinu ya TANESCO inayopeleka umeme wa gridi mkoa Kigoma


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI