Header Ads Widget

WAZIRI AWESSO AWAPONGEZA BONDE LA MTO RUVUMA NA PWANI YA KUSINI

 


Mtwara, 


Waziri wa Maji Jumaa Awesso amewapongeza Bonde la Mto Ruvuma na Pwani ya kusini kwa kuboresha miundombinu ya ofisi yao sambamba na kuweka maabara ya kupimia maji ambayo awali walikuwa wakifanya vipimo hivyo Dar es salaam. 


Akizindua jengo hilo alisema kuwa ni muhimu maabara kuanza kutumika  ambapo zitaepusha gharama zilizokuwa zikitumika awali hivyo kuongeza ufanisi wa kazi. 



"Mkianza kupima maji hapa mtaepusha vitu vingi hivyo kurahisisha kazi zenu ikiwemo kupima parameter mkumbuke kuwa mnajitegemea sio wakala vifaa vyote  muhimu viletwe ili kazi uendelee"


"Wapo watu wanabeza kuwa Mtwara hakuna maji nendeni mkatumie utalaamu wenu  fanyeni tafiti za kutosha penye maji chimbeni watu wapate huduma ya maji huduma ya maji ni muhimu kwa kila mtu"



Kwa upande wake MKurugenzi wa Bonde la Mto Ruvuma na Pwani ya Kusini Sudi Mpemba amesema jengo hilo la ofisi ya Mtwara pamoja na mengine ya Lindi na Ruvuma yamegharimu zaidi ya shilingi Bilioni 2.5. 


Aidha amesema kukamilika kwa majengo hayo kutawapa utulivu watumishi na kuwafanya wafanyakazi katika sehemu salama ambapo tunajukimu kubwa la kufanya tafiti za rasilimali za maji juu na chini ya ardhi. 


"Waziri amekuja Kuangalia miradi mbalimbali inayotekelezwa kwa ngazi za mabonde ambapo tunayo mipango ya kutunza na kuainisha vyanzo ya maji ambapo mpaka sasa tumebaini vyanzo 58  tumesha hifadhi vyanzo  13 vimehifadhiwa kwa hatua mbalimbali mfano chanzo cha Mbwinji tumeelimisha jamii kuacha shughuli hatarishi kando ya vyanzo vya maji" alisema Mpemba


MWISHO

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI