Header Ads Widget

MIKOA MITANO TANZANIA HATARINI KUPATA EBOLA

 


Na fatma Ally Matukio Daima APP Dar es Salaam


Serikali imesema licha ya kutokuepo kwa mgojwa wa ebola lakini Tanzania ipo katika tishio la kupata ugonjwa huo huku ikiwataka wananchi kuchukua tahadhari ikiwemo kunawa na maji tiririka, kuepuka kula nyama mbichi, mizoga pamoja na kwenda sehemu ambazo zina wagonjwa wa ebola.


Aidha, imewataka wakuu wa Mikoa yote nchini kuchukua Tahadhari namna gani ya kukabiliana na tatizo hilo ikiwemo kuweka mazingira mazuri endapo mgonjwa wa ebola atapatikana, waangalia daktari gani atakae mtibia, gari gani itambeba na sehemu gani wataweza kumueka kwa ajili ya kupata matibabu.


Katika taarifa iliyotolewa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Afya Ummy Mwalim mbele ya waandishi wa habari imesema kuwa , kuwepo kwa ugonjwa huo nchi jirani kunaieka Tanzania katika hatari ya kupata ugonjwa huo kutokana na muingiliano wa mkubwa wa shughuli za kiuchumi na kijamii na mikoa ya Kagera, Kigoma, Geita, Mwanza na Mara kwa kutumia mipaka rasmi na isiyorasmi.


"Nina waagiza wakuu wa mikoa yote kila Halmashauri kuandaa mpango wa kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa huu, kuimarisha ufuatiliaji na kutoa taarifa ya wahisiwa wenye dalili za ugonjwa huu,pia waganga wakuu wa mikoa kuhakikisha wanatoa taarifa sahihi na Kwa wakati kwa mganga Mkuu wa Serikali kuhusu tetesi za wahisiwa na mwenendo wa ufuatiliaji wa ugonjwa huu"amesema Waziri Ummy.


Aidha, amesema hatua mbalimbali zimeendelea kuchukuliwa na Serikali Ili kuzuia ugonjwa huo kuongia nchini Tanzania ikiwemo kuimarisha utayari wa kukabiliana na ugonjwa huo kwa kuimarisha uchunguzi wa wasafiri katika mipaka hasa yenye muingiliano mkubwa na nchi ya Uganda - Mutukula, Dar es Salaam , Kilimanjaro, Kigoma na Mara.


Hata hivyo,amesema endapo mtu atabainika na dalili ya homa kali, kuharisha, kutapika, mwili  kuchoka, kutokwa damu katika matundu ya mwili yaani mdomoni, maskioni, machoni na njia ya haja kubwa na ndogo ni vyema kukimbizwa hospitali haraka kwa ajili matibabu kwani anaweza kufariki ndani ya muda mfupi

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI