Header Ads Widget

MEYA WA JIJI LA MWANZA SIMA AZINDUA TAASISI YA WANAWAKE WACHAKATAJI WA SAMAKI KANDA YA ZIWA



Msitahiki Meya wa Jiji la Mwanza Mhe. Sima Constantine amefungua kikao cha kuimalisha Taasisi ya Wanawake Wachakataji wa Samaki  ( TAWFA ) Kanda ya Ziwa katika Ukumbi wa Nyakahoja kanisani Mwanza 



Wanawake Wachakataji wa Samaki Kanda ya Ziwa ( TAWFA ) wamesema changamoto kubwa inayowakabiri ni upatikanaji wa Masoko,Unyanyasaji wa kingono pamoja na matumizi ya lugha zisizo na staha kutoka kwa wavuvi wakiwa mwaloni pamoja na wenza majumbani pale wanapohitaji msaada wa kifedha



Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza,Sima Constantine amesema, Uzinduzi wa Taasisi ya Wanawake Wachakataji wa Samaki (TAWFA ) Kanda ya Ziwa inakwenda kugusa kundi kubwa la Wanawake wanaofanya uvuvi mdogo, ikiwa ni fursa kubwa kwa nchi katika kuelekea uchumi wa Buluu katika kutumia rasimali ya Maji 



Mkurugenzi wa Emedo Editrudith Lukanga, amesema ufunguzi wa Taasisi ya Wanawake Wachakataji wa Samaki (TWFA) kanda ya ziwa itakwenda kukuza uelewa utakaosaidia kujenga mazingira wezeshi kwa ajili ya uendelevu wa uvuvi kwa manufaa ya wavuvi wadogo na kufanya jamii kutambua na kuthamini mchango wa wanawake katika uvuvi.



Aidha wanawake hao wamechagua uongozi wa taasisi hiyo kwa kanda ya ziwa ambapo Jovitha Juston kutoka Kagera Muleba amefanikiwa kushinda nafasi ya uenyekiti huo huku Kalunde Joseph akipata nafasi ya umakamu uenyekiti wa taasisi hiyo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI