Header Ads Widget

MAMA AKAMATWA KWA MAUAJI NJOMBE

 


Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE


Jeshi la polisi mkoa wa Njombe linamshikilia Happines Mkolwe[27] mkazi wa kijiji cha Ihanga halmashauri ya mji wa Njombe mkoani Njombe kwa tuhuma za mauaji ya mtoto Jackson Kihungo mwenye umri wa miaka 6 wa  mama aliyekuwa na mahusiano na mumewe. 


Mbele ya vyombo vya habari kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Hamis Issah amesema mtuhumiwa huyo baada ya mahojiano amekiri kutekeleza mauaji hayo baada ya mumewe ambaye waliachana kudaiwa kuwa na mwanamke mwingine.


Wivu wa mapenzi ndio unaotajwa kusababisha ukatili huo uliosababisha mauaji ya mtoto huyo wa darasa la kwanza katika shule ya msingi Ihanga ambapo Happiness alimchukua mtoto huyo wakati akitoka saluni kunyoa na kwenda naye polini wanakopasulia mbao na kisha kumuuwa na kumfukia kwenye masalia ya mbao.


Sanjari na tukio hilo lakini pia Kamanda Issa amewataka wananchi wote wanaomiliki silaha kinyume cha sheria kuzirejesha kwenye mamlaka zinazohusika katika kipindi hiki cha mwezi septemba kabla msako mkali haujaanza.


Baadhi ya wakazi wa Njombe akiwemo Lukule Mponji wamesema vijana ndio wamekuwa na tabia ya kujihusisha kimapenzi bila utaratubu mzuri na ndio chanzo kinachosababisha mauaji hayo.


Juu ya usalimishaji wa silaha wanasema hatua hiyo ya jeshi la polisi ina dhamira njema kwani itasaidia sana kupunguza vitendo vya kihalifu vinavyofanywa kwa kutumia silaha hizo huko uraiani.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI