Ijazaji huu za mazao ya misitu ni hatari Kwa barabara ya lami kati ya Sawala, Luhunga na Iyegea wilaya ya Mufindi mkoani Iringa
Hili ni eneo lililoharibiwa na Lori ambalo lilizidisha mzigo na taili kupasuka hivyo kutembelea lim WANANCHI wa vijiji vya Sawala ,Luhunga na Iyegea katika wilaya ya Mufindi mkoani Iringa wamepongeza ujenzi wa wa barabara ya kiwango cha toka Sawala, Mkonge, Igoda, Ikaning'ombe na yegeya kuwa umesaidia sana kero ya usafiri japo wameomba serikali kuwabana wanye malori yanayobeba mizigo mizito kupita uwezo wa barabara hiyo .
Wakizungumza na matukio Daima App juzi wananchi hao walisema pamoja na jitihada kubwa zinazofanywa na serikali na wahisani kujenga barabara hiyo kwa kiwango cha lami ila changamoto kubwa wanayoiona ni malori ya mazao ya misitu ambayo baadhi yamekuwa chanzo cha kuharibu barabara hiyo .
Frank Ndelwa mkazi wa Luhunga alisema ili barabara hiyo iendelee kuwa bora ni vema kuwepo kwa sheria kali kwa wamiliki wa malori yatakayobainika kuzidisha mizigo na kupita kwenye barabara hiyo .
Kwani alisema kampuni za ujenzi ambazo zinaendelea kufanya kazi ya kukamilisha ujenzi hiyo pamoja na kufanya kazi kwa kiwango ila kama hakutakuwa na usimamizi na sheria kali za kulinda miundo mbinu ya barabara hiyo kazi hiyo itakuwa ni bure maana muda mfupi barabara itakuwa imeharibika .
Ajuaye Sanga mkazi wa Sawala na mwisho kijiji cha Iyegea alitaka mwanzo wa barabara eneo la Sawala kuwepo kwa tangazo linaloonesha gari tani ngapi linatakiwa kupita kwenye barabara hiyo na aina ya adhabu ambayo itatolewa kwa mkiukaji wa agizo lililowekwa .Kuwa kazi ya kusimamia sheria hiyo inapaswa kufanywa na serikali za vijiji vyote vinavyopita barabara hiyo ili kuona miundo mbinu ya barabara inalindwa na barabara inabaki kubwa mkombozi wa wakulima wa mazao mbali mbali yanayozalishwa na wakulima wa ukanda huo kama miti ,chai na mazao mengine ya chakula.
Alisema barabara hiyo itakuwa ni mkombozi kwa wakulima wa chai waliokuwa wakipoteza mazao yao kwa kushindwa kufika kiwandani kwa wakati kutokana na ubovu wa barabara hasa kipindi cha masika
0 Comments