Header Ads Widget

KLINIK INAYOTEMBEA YAWAFIKIA WANANCHI ZAIDI YA 30000 KATIKA KUTOA HUDUMA ZA AFYA

Na Teddy Kilanga, MatukioDaimaAPP Arusha 

Kutokana na baadhi ya wananchi kufika katika vituo vya afya wakiwa wamechelewa kupata matibabu ya  maradhi yanayowasumbua,Kliniki inayotoa huduma za afya mchanganyiko za kisasa na asili iliyochini ya Taasisi ya Amin Preventive and Healing Clinic imeanza kuwafikia jamii ya pembezoni ya hifadhi yaTaifa ya Arusha kwa lengo la kuwapatia elimu juu ya umuhimu wa kupima afya zao kila mara.

Taasisi hiyo imeshawafikia wananchi zaidi ya 30000 ikiwa nusu ya hiyo wamekutwa na maradhi mbalimbali nakuanzishiwa huduma za afya na wengine kupatiwa tiba za asili ikiwemo matumizi sahihi ya vyakula.

Akizungumza na vyombo vya habari Mganga mkuu wa kituo hicho,Dk Baraka Barati amesema wananchi wengi wamejijengea tabia yakufika katika vituo vya afya ikiwa viwango cha maradhi vimeshafikia hatua mbaya lakini wakipewa elimu juu ya umuhimu wa kupima afya mapema inawasaidia kutambua na kudhibitwa kwa wakati.

"Sisi tunashughulika na kupima magonjwa mbalimbali  ikiwemo saratani ya mlango wa kizazi,Kisukari ,vidonda vya tumbo,magonjwa ya mifupa ,vidonda sugu,presha,Tezi dume pamoja na macho na tunapowafuata katika makazi yao huwa tunawaelimisha kisha kuwaanzishia huduma za matibabu,"amesema Dk.Barati.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa kituo hicho,Dk.Cornelia  Wallner Frisee amesema kliniki yake imeamua kufanya  hivyo kutokana na changamoto ya baadhi ya watanzania kutokuwa na tabia ya kupima hadi pale watakapokuwa wamezidiwa na maradhi yanayowasumbua.

"Ningependa kuwashauri watanzania kutenga siku moja katika mwaka kwa ajili ya kuangalia afya yako hata kama hawaumwi au huna dalili za ugonjwa kwani itamsaidia mtu yoyote kubakia salama katika kuweza kitunza afya yako,"amesema.

Aidha ameongeza kuwa mbali na kutoa huduma za kiafya wanatoa elimu kwa wananchi juu ya mifumo mbalimbali ya maisha ambayo wanaweza kuwasaidia kutunza afya zao.

Pia aliishauri jamii hiyo kula vyakula vya asili vinavyojenga mwili pamoja na kufanya mazoezi mbalimbali ya tiba kwani inasikitisha kuona baadhi ya watu wanateseka kwa ugonjwa wa misuli au viungo hali inayopelekea kushindwa kufanya shughuli za kila siku kutokana na kukosa  tiba sahihi.

 Nao baadhi ya wananchi waliofikiwa na huduma hiyo wameiomba serikali kuweka mikakati ya utoaji wa elimu ya matumizi sahihi ya tiba asili inayoathiriwa na mtindo wa maisha ikiwemo ulaji mbovu wa vyakula.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI