NA THABIT MADAI, MATUKIO DAIMAAPP ZANZIBAR
KIJANA Mmoja anaefahamika kwa Jina la Mohammed Mzee miaka 27 Mkazi wa Zanzibar ameeleza kuwa ameacha kutumia Dawa za Kulevya aina ya Bangi mara baada ya kushiriki katika Kilimo cha Vanila ambacho kimebadilisha Maisha yake.
Ameeleza kwa takribani miaka 10 amekuwa akitumia bangi pamoja na kuishi maisha ya maskani ambapo hakuwa na muelekeo katika Maisha yake.
“Kiukweli sikuwa kwa Miaka mingi nilikuwa naishi maisha ya Maskani na kutumia Bangi ila baada ya kushawishiwa kujiunga na Kilimo cha Vanila nimeacha kutumia na sasa naelewa mustakabali wa Maisha yangu,” ameeleza.
Ameongeza kwamba kilimo hicho kina mfanya anakuwa anakuwa na Shughuli nyingi na kukosa muda wa kukaa Maskani na kutumia bangi na starehe nyingine.
Ameeleza kwa sasa anauhakika wa kuingiza kiasi kisichopungua Laki 350 na kuendelea baada ya kuingia katika kilimo hicho ambapo anashirikia katika shamba la Vanila Internation Limited Zanzibar huko bungi.
“Tulishawishiwishiwa vijana wengi kuingia katika Vanila ila wengine wakakataa sasa baada ya kuingia kwa muda mfupi nimeona faida yake naingiza kiasi kikubwa na kusaidia familia yangu,”amesema.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Vanila International Limited Simon Mkodya ameeleza kuwa kuna vijana wengi wa mitaani wamewasaidia kuwaingiza katika kilimo na kuwasaidia kujikwamua na Maisha.
“Kilimo hichi kina faida kubwa sana na kwa Mtu Mmoja Mmoja na taifa kwa ujumla ambapo vijana wengi sasa wananufaika,” amesema.
Amesema Kilo Moja ya Vanila kwa sasa ni laki Nne na Hadi Laki Tano na zao lake linadumu kwa kwa takribani miaka 60.
Ameongeza kwamba, Katika Shamba hilo amewaamewaajiri Vijana takribani 270 katika kilimo hicho na anawakaribisha Vijana wengine kushiriki katika Kilimo hicho.
0 Comments