NA MATUKIO DAIMA MEDIA,
Katika tukio lisilo la kawaida mtu mmoja mjini hapa
anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kosa la kubaka, na kumsababisha mauti.
Kwa mujibu wa shuhuda ambaye ni shemeji wa marehemu
anasema siku ya tukio akiwa anatoka kwenye shughuli zake alikuta mazingira
tatanishi na baada ya kuingia ndani ndipo mtuhumiwa alichoropoka na kukimbia.
Anasema kwa mujibu wa mtoto wa marehemu kuwa mtu huyo
alifika nyumbani hapo kisha kumvamia mama yake na kumfanyia kitendo hicho
ambacho kilipelekea mama huyo kufikwa na umauti.
Nae mme wa marehemu Bwana Adeline Michael Kileo
akizungumza na Matukio Daima Media kwa uchungu amesema mkewe alikuwa mjamzito
na walitarajia kupata mtoto wa pili, anasema siku ya tukio mkewe alirudi kazini
ila kutokana na hali yake akamuomba amsaidie kazi, mme wa marehemu anaendelea
kueleza kuwa wakati tukio hilo likitendeka yeye akuwepo na aliporejea alikuta
tayari mkewe ametendewa unyama huo na kijana anayeitwa Mohamed Mwanjali.
Nae Balozi wa Mtaa wa Maweni Bwana Yassin Salum
Kisogole anasema alipokea taarifa toka kwa mme wa Marehemu juu ya tukio na
ndipo alipoongozana na kijana na polisi kumkamata mtuhumiwa.
Jeshi la polisi bado linaendelea na uchunguzi wa tukio
hilo wakati mtuhumiwa akiwa chini ya ulinzi wa jeshi hilo mkoani hapo.
Tukio hilo limetokea Usiku wa kuamkia Jumapili ya
Tarehe 25/09/2022 katika mtaa wa Maweni, Kata ya Kitanzini Mjini Iringa.
0 Comments