Header Ads Widget

WAZAZI WENYE WATOTO WALEMAVU WAASWA KUELEKEA SENSA YA WATU NA MAKAZI

 





NA HADIJA OMARY _Matukiodaima App LINDI..



Kuelekea siku ya Sensa ya Watu  na makazi inayotarajiwa kufanyika hapo kesho August 23, 2022 hapa Nchini Tanzania Wazazi na walezi kutoa taarifa sahihi za Watoto wenye mahitaji maalumu wanaoishinao katika familia zao ili kuirahisishia Serikali kupanga mipango ya kimaendeleo ikiwemo Bajeti sahihi kwenye sekta ya Elimu.




Wito huo umetolewa na ofisa Elimu, Elimu maalumu Henry Helahela alipokuwa anazungumza na matukio daima ofisini kwake akieleza juu ya umuhimu wa Sensa ya watu na makaazi utakavyoifanya Serikali na wadau wengine kupanga Bajeti sahihi katika sekta ya Elimu kwa Watoto wenye ulemavu




Helahela alisema kuwa kupatikana kwa takwimu sahihi za Watoto wenye mahitaji maalumu zitasaidia kwa kiasi kikubwa kuainisha mahitaji  halisi ya Watoto wenye ulemavu kwa kipindi cha sasa na baadae.




“baada ya kupata Takwimu sahihi  Itaifanya serikali   kupanga mipango inayowanufaisha watu wenye ulemavu ikiwemo Watoto katika sekta ya Elimu hasa swala la miundombinu rafiki kwa Watoto wenye mahitaji , Walimu wataalamu ambao wamesomea Elimu maalum ambayo itaenda sambamba na idadi ya Watoto waliopo ndani ya halmashauri husika ambalo litafanywa baada ya kupata zile takwimu kwenye zoezi la Sensa”.  Alisema Helahela




Helahela aliongeza kuwa Serikali ilipoamua kufanya Sensa kila baada ya miaka kumi ilikuwa na lengo  la kuweza kubaini idadi ya watu wa kuwahudumia kwa ajili ya  kutoa huduma kwa wananchi inayoenda sambamba na mipango iliyohusisha takwimu sahihi za Wananchi katika Eneo husika.



“miongoni mwa watu hao wanaotakiwa kupata huduma ni watu wanye mahitaji maalumu ikiwemo na Watoto, vijana na watu wazima (wazee)  ambapo kutokana na aina mbali mbali za ulemavu huo kama vile viziwi, wasioona, wenye ulemavu wa akili , ulemavu wa viungo na pia watu wenye ualubino watahitaji visaidizi na wasaidizi”




Kwa upande wake Mwalimu wa kitengo cha Watoto wenye ulemavu wa akili Shule ya Msingi Namakonde iliyopo Halmashauri ya Ruangwa Mkoani Lindi  Janeth Mwambe alisema kuwa moja ya changamoto wanayokabiliana nayo katika Shule hiyo yenye Watoto wenye mahitaji maalumu ni vifaa vya kufundishia na kujifunzi.



Alisema endapo wazazi na walezi watakuwa na hamasa ya kutoa taarifa sahihi ya Watoto walemavu wanaoishi nao katika maeneo yao itaifanya Serikali kutambua mahitaji sahihi ya Watoto ikiwa Pamoja vifaa hivyo vya kufundishia na kujifunzia




“ kwa mujibu wa Serikali Shule hii inatambulika kuwa ni Shule ya Watoto wenye mahitaji maalumu ya walemavu wa akili lakini kutokana na hamasa ya wazazi kutaka kuwaleta Watoto wao hapa hata wale Watoto wenye changamoto zingine tumekuwa tukiwapokea na kufanya idadi ya wanafunzi hawa ikiongezeka mwaka hadi mwaka” 




“hapa tunaanza kupokea Watoto wa miaka mitano na tulianza kupokea wanafunzi mwaka 2012 tukiwa na wanafunzi watano ambapo idadi hiyo imeongezeka mpaka kufikia 32 kwa mwaka huu 2022 kati yao wasichana 18 na wavulana 14" 



Amina Juma mama wa Mtoto Baraka mwenye miaka (06)  mkazi wa Kijiji cha Mchanama Halmashauri ya Ruangwa Mkoani Lindi, alisema kuwa upo umuhimu wa watoto waliopo kwenye kundi hilo kuhesabiwa kwa sababu itasaidia Serikali kupata takwimu sahihi Watoto walemavu.




“mwanangu Baraka mwenye ulemavu wa viungo (alizaliwa akiwa hajatimia viungo kwenye mikono yake) ni mwanafunzi katika shule ya msingi Namakonde iliyopo Wilayani Ruangwa lakini kutokana na ulemavu wake anashindwa kuudhuria vipindi kwa wiki mzima kutokana na umbali wa shule anayosoma kutokea tunapoishi nashindwa kumpeleka kwa wakati ”



"Kutokana na changamoto ninazozipitia mimi kama mzazi katika kumuhudumia Baraka wakati wa kumpeleka Shuleni naona Sensa ni muhimu ili kuisaidia Sarikali kupata taarifa sahii za Watoto wenye ulemavu na mahitaji yake   kwani inaweza kuona umuhimi hata wa kujenga mabweni ili watoto waweze kuishi pale shuleni” 



"Kwa mfano kuna makundi kama ya akina Baraka ni walemavu wazazi wasiwafiche ndani wawatoe nje nao wahesabiwe wasiwanyime haki zao za msingi ili kuifanya Sarikali kutambua Watoto walemavu wapo wangapi, na wanahitaji nini ili ijue namna ya kuwasaidia"  Amina



Kwa upande wake Mjumbe  wa chama cha Watu wenye ulemavu Mkoa wa Lindi, Hamisi Mohamed (Madenge) alisema kuwa kundi la watu wenye ulemavu ni Sawa na Makundi mengine hivyo yanapaswa kuhesabiwa 




"Kwa mujibu wa Sheria ya Takwimu sura Namba 351 ni wajibu kisheria kwa wananchi kujibu maswali ya Sensa kwa karani hivyo ni wajibu wa watu wote kutoa ushirikiano kwa makarani wa Sensa ya watu na makazi 2022 kwa kutoa taarifa sahihi ili kurahisisha na kufanikisha zoezi hilo 



" Matokeo ya Sensa yatachochea kasi ya maendeleo ya Watu na makazi yao katika maeneo yote ya utawala hapa Nchini bila kuja hali ya mwananchi huyo kuwa ni Mlemavu au laa"


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI