Header Ads Widget

WATUMIAJI WA ARIDHI WAMETAKIWA KUPIMA MAENEO YAO ILI KUONDOA MIGOGORO

 





NA HADIJA OMARY,MATUKIO DAIMAAPP

LINDI


ILI kuepukana na migogoro inayotokana na Watumiaji wa  Aridhi Watanzania wametakiwa kufuata taratibu za umiliki wa Maeneo yao ikiwa ni pamoja na kuyapima na kupata hati miliki


Wito huo umetolewa na ofisa mipango miji kutoka Wizara ya Aridhi Nyumba na maendeleo ya makazi Evalina Kiria katika maonyesho ya wakulima (nane nane ) yanayoendelea katika viwanja vya maonyesho Ngongo Manispaa ya Lindi mkoani humo.


Kiria alisema kuwa  ili kukwepa Migogoro hiyo ni jukumku la kila mwananchi na mtumiaji wa Aridhi kuhakikisha  anafuata taratibu na sheria za kumiliki Aridhi.


Alisema asilimia kubwa ya watumjiaji wa Aridhi ufanya shughuli zao edha kwa makazi ya kuishi ama shughuli za kilimo pasipo kufahamu kama Eneo hilo limepimwa ama vinginevyo.


“Wito wangu kwao  ni wao kuwa na ile kiu kujua ni namna gani wanamiliki maeneo yao ili zile Aridhi wanazozitumia wazimiliki kihalali”

 

Kwa upande wake Ofisa Aridhi Mteule wa Manispaa ya Lindi Andrew Munisi, alieleza miongoni mwa sababu zinazopelekea kuwepo kwa Migogoro ya Aridhi ni kutokupimwa kwa Aridhi kunakosababisha mtumiaji wa Aridhi hiyo kutokufahamu mipaka ya eneo lake , migogoro ya wakulima na wafugaji ambayo kwa kiasi kikubwa utokana na kugombea maeneo ya kulishia.


“ili kukabiliana na haya yote mfano kwenye migogoro inayohusu mipaka hivi sasa idara ya Aridhi tumekuja na vifaa maalumu vya kugawa  maeneo baina ya kiwanja na kiwanja changamoto tuliyokuwa nayo katika eneo hili ni watumiaji hao wa Aridhi kujiwekea mipaka yao ya kienyeji,  utakuta watu wanajiwekea alama ya mgomba mpakani sasa ule mgomba siku ukifa ndio basi mpaka umepotea, kwenye migogoro ya wakulima na wafugaji pia tumeweza kupunguza migogoro kwa kupanga mipango ya matumizi bora ya Aridhi kwenye vijiji” alisema Munis

 

Migogoro mingine husababishwa na baadhi ya wataalamu wasio waaminifu ambao ugawa kiwanja kimoja kwa watu Zaidi ya mmoja , migogoro inayosababishwa na viongozi wa Serikali za Mitaa kuvamia maeneo ya watu na  kuuza kwa watu wengine bila hidhini ya miliki, na mingine ni ile ambayo watu ama mtu kutolidhika na fidia.


Akizungumza baada ya kupata maelezo mafupi ya shughuli zinazofanywa na Wizara hiyo katika Banda la Wizara ya Aridhi Nyumba na maendeleo ya Makazi   (Nane nane) Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Abbas Ahmed aliipongeza Wizara hiyo kwa namna ilivyoweza kupunguza Migogoro ya Aridhi hapa Nchini


"Mapinduzi makubwa kwenye eneo la Aridhi ambalo kwa kipindi kirefu lilikuwa na migogoro lakini ndani ya muda mfupi baada ya kuingia damu mpya naona kasi yenu imeongezeka ya kutatua hiyo migogoro hongereni sana , lakini pia utoaji wa hati ambayo pia ilikuwa ni kilio kikubwa kwa wananchi "


"SISI viongozi wa kiutawala tunaipongeza wizara kwa kiwango kikubwa Hongereni sana, msibweteke na sifa endeleeni na kasi hiyo kwa sababu hii Aridhi ni Raslimali ambayo unaweza ukaikopea ukapata hela ukafanyia miradi mingine mwananchi asipofikia lengo hilo ninyi ndio mmesababisha asifike". Alisema kanali Ahmed 


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI