Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema serikali itaendelea kuboresha huduma za afya ukiwa ni utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi mkuu katika kuwahudumia wananchi.
Rais Samia ametoa kauli hiyo alipotembelea na kukagua jengo la mama na mtoto katika Hospitali ya Rufaa mkoa wa Njombe na kwamba serikali itaendelea kupambania afya za wananchi kwa kujenga miundombinu mizuri na yenye kuleta ustawi mzuri wa jamii.
Ummy Mwalimu ni waziri wa afya ambaye amesema hadi Sasa Hospitali hiyo imetumia kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 27 na wodi za mama na mtoto zitalaza wagonjwa 150.
Amesema jengo hilo kitakapokamilika litasaidia sana kupunguza adha kwa akina mama katika kutafuta huduma za afya umbali mrefu huku akiwataka wananchi kuendelea kukata bima za afya zinazopunguza usumbufu wakati wa kutafuta huduma za afya.
0 Comments