Header Ads Widget

WANANCHI KIBAHA WATAKIWA KUSHIRIKI ZOEZI LA SENSA

 



WANANCHI wa Wilaya ya Kibaha wametakiwa kushiriki zoezi la sensa 23 mwezi huu ili waweze kupata mgawanyo sawa wa rasilimali za maendeleo kwani kwa sasa hauko sawa kutokana na kutokuwa na takwimu sahihi za watu.



Hayo yamesemwa Mlandizi Sara Msafiri wakati akizungumza na viongozi wa madereva bodaboda, viongozi wa soko na wausafirishaji wa daladala katika kikao cha kujadili namna ya kuhamasisha watu kushiriki sensa.



Msafiri amesema ili mgawanyo uende sawa na kila mmoja apate huduma stahiki ni vema wananchi washiriki kuhesabiwa  ili Serikali iweze kupeleka huduma inayoendana na idadi ya watu.



"Rais amewekeza kwenye anuani za makazi na sensa ya watu wananchi tutoe ushirikiano kwa makarani wa sensa, nimewaita nyie ili mnisaidie kuhamasisha na wataalamu wataendelea kutoa elimu kila mahali kuhusiana na umuhimu wa hili jambo,"amesema Msafiri.



Aidha amewataka wafugaji kuondokana na dhana ya kwamba mifugo ikihesabiwa inakufa badala yake waruhusu kuhesabiwa wao na mifugo yao ili dawa za mifugo ziweze kutolewa za kutosheleza idadi iliyopo.



Mkuu huyo wa Wilaya amemuelekeza ofisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Kibaha kuitisha kikao na wanawake ili waweze kupatiwa elimu ya sensa kwani wao ni watu wenye ushawishi kwenye jamii.



Naye Mkufunzi wa sensa wa Halmashauri hiyo Gele Msangi aliwataka wananchi kuzingatia kutoa taarifa sahihi kwa makarani wa sensa.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI