Header Ads Widget

AMCOS YA MAHENGE WILAYA YA MBINGA YAWALIPA FEDHA WAKULIMA 58 WA ZAO LA KAHAWA



***********

AMON MTEGA, MBINGA.

CHAMA cha msingi cha Mahenge (Mahenge AMCOS) Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma kimeshamaliza kuwalipa fedha wakulima 58 wa zao la Kahawa ambao hawakulipwa kwenye malipo ya awali kutokana na makato ya kurejesha mkopo wa mashine ya kukobolea kahawa iliyopelekwa kwenye Kijiji cha Langandondo.

Akizungumza mwenyekiti wa chama hicho Julius Mbunda wakati malipo hayo amesema kuwa wakulima hao walikuwa wamesalia takribani zaidi ya miezi minne kwenye Malipo ya awali wakati wa uuzaji wa kahawa hiyo wote wameshalipwa.

Mwenyekiti Mbunda amefafanua kuwa sababu za wakulima hao kushindwa kulipwa malipo yao kwa wakati ni kufuatia deni ambalo lilikopwa benki kwaajili ya kununulia mashine mbili za kukobolea kahawa katika Kijiji cha Mahenge na Kijiji cha Langandondo wakati wakitumia AMCOS moja na kuwa kabla ya halijalipwa deni hilo Kijiji cha Langandondo kilikuwa kimefanikiwa kupata AMCOS yake hivyo malipo ya kahawa yalipoingia benki ,yalikatwa kwa jina la wakulima wa Mahenge kutokana na mkopo huo kuwa na jina la Mahenge.

Amesema kuwa AMCOS hiyo ambayo inasoko la kuuzia kahawa ndani ya Nchi na Nje ya Nchi ambao wadau wao wa soko la Nje ni wakutoka Ujerumani wakitumia kampuni ya Parterkaffee iliingiza fedha za malipo kwa wakulima wote kutokana na mkataba waliyowekeana hivyo makato yalifanyika benki kutokana na deni hilo.

Ameeleza kuwa kwa sasa wakulima 58 waliyokuwa wamesalia wameshalipwa kwa jitihada za Chama hicho huku akiwataka baadhi ya wakulima hao kufungua akaundi(ACCOUNT)Benk ili kuwalahisishia msimu ujao wa mauzo walipwe fedha zao kupitia kwenye mfumo wa kibenk.

Kwa upande wake mmoja wa waliyepokea malipo hayo Theudos Mbepera amesema anakipongeza chama hicho kwa kuwapigania malipo hayo na kuwa baadhi yao walishakata tamaa kuwa hawatalipwa jambo ambalo limewatia moyo yeye na wenzake kuendelea kuuamini ushirika katika suala Zima la kumkomboa mkulima.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI