Header Ads Widget

VIJANA LINDI WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA GESI ASILIA

 





NA HADIJA OMARY LINDI....


VIJANA  wa Mikoa ya Lindi na Mtwara wametakiwa kuhamasika kusoma Taaluma za maswala ya Gesi na Mafuta yanayotolewa na vyuo vya ufundi stadi (VETA) vilivyopo kwenye maeneo yao ikiwa ni kujiandaa na fursa za ajira zitakazotokana na ujio wa mradi wa uchakataji Gesi Asilia ya (LNG)



Wito huo umetolewa na mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa Shirika la maendeleo ya Petrol Tanzania (TPDC) Balozi Ombeni Sefue alipokuwa anazungumza katika kikao cha kujitambulisha kwa viongozi wa Mkoa huo wa Lindi kilichofanyika katika ukumbi wa Mkuu wa mkoa huo ikiwa ni miezi michache baada ya bodi hiyo kuteuliwa.



Balozi Sefue akiwa na wajumbe wengine wa Bodi ya TPDC  walitembelea eneo la Likong'o ambako mradi huo wa uchakataji wa Gesi asilia utatekelezwa.




Sefue alisema Serikali ilipoamua kuvifanya vyuo vya ufundi stadi (VETA) vya Mikoa ya Lindi na Mtwara kufundisha maswala ya Gesi ilidhamiria kuwaandaa vijana kuwapa ujuzi utakaowawezesha kuajiriwa kwenye mradi huo pindi utakapokamilika.



“itakuwa ni jambo la kushangaza kuona vyuo hivi vinafundisha maswala ya gesi lakini ukakuta vijana wenyewe wa Lindi wanaosomea masomo hayo ni asilimia 3% au 2% ndio vijana wanaotoka maeneo haya , kwa hivyo ni vizuri vijana waelewe kwamba kunufaika ni lazima wajiandae” alisisitiza Balozi Sefue



Alisema faida ya kuduma kwa wananchi inatokana na sehemu ambayo mradi wenye unapotekelezwa ambapo utaunganishwa na shughuli zinazotokana na mradi huo kama vile ajira kwa vijana katika Eneo la mradi Pamoja na biashara za ujasiliamali.




“ huko nyuma tulikuwa tuna kitu kinaitwa CSR anakuja mwekezaji mkubwa anakuambia anakujengea madarasa Mawili au Zahanati anafikiri wajibu wake umeisha lakini sisi kama Serikali lazima tufikirie Zaidi ya hayo kwamba faida hasa ni nini? Na faida ya kudumu inatokana na  uchumia unaotokana na pale ambapo mradi upo” alisema.


 

Awali akieleza utekelezaji wa Mradi huo Mkuu wa Wilaya ya Lindi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo Shaibu Ndemanga alisema kuwa wao kama Mkoa kwa kushirikiana na TPDC wamekuwa na Program mbali mbali zinazohusiana na Gesi  katika kuhakikisha wanaendelea kutoa Elimu na uhamasishaji kwa jamii .



Alisema kupitia Program hizo Chuo cha ufundi Stadi (VETA) cha Mkoa wa Lindi na Mtwara tayari vimeanza kupokea wanafunzi  wa mikoa hiyo kupitia mpango wa ofisi ya Waziri Mkuu ambapo vijana wapo kwenye vyuo hivyo wakipata mafunzo kwa fani tofauti tofauti .


“kwa upande wa wananchi tumewaandaa vzuri kama tulivyosema, tumekuwa na mikutano na wadau mbali mbali kama vile wenye mahotel, wamiliki wa Nyumba pamoja na watoa huduma wengine kuwaweka tayari kutoa huduma  wakati wa mradi unaendelea” alisema Ngemanga

 

 


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI