Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi amefanya ziara ya kikazi katika Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya kwa lengo la kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na Wakala wa Maji Vijijini(RUWASA) ambapo katika Kijiji cha Mkunywa Kata ya Madibira ametembelea mradi wa maji uliokwama kwa miaka kumi na mbili.
Mradi huo aliouita kichefuchefu Naibu Waziri wa Maji amepokea taarifa kutoka kwa Meneja wa RUWASA Wilaya ya Mbarali Samwel Heche ambaye amesema mradi umepokea zaidi ya shilingi milioni mia nane na utakapokamilika utanufaisha vijiji saba vikiwemo Iheha,Mahango,Chalisuka,Mkunywa,Ikoga,Nyamakuyu na Nyakadete.
Diwani wa Kata ya Madibira Juma Msiminyungu amesema tangu kujengwa tanki hilo lililogharimu shilingi milioni 90 miaka 12 iliyopita halijawahi kupokea maji.
Aidha baada ya ukaguzi Mahundi ameongea na wananchi wa Kijiji cha Mkunywa ambapo Sesi Chungu,Consolata Mwinuka,Aplon Kinyanga na Alunesi Kayoka wamesema baadhi ya wanawake ndoa zao zipo mashakani kwa kuwa muda mwingi wanautumia kutafuta maji makorongoni.
"Mheshimiwa Naibu Waziri mimi niliumia mguu baada ya kuanguka korongoni nikichota maji"alisema Consolata Mwinuka huku akipiga magoti mbele ya Naibu Waziri akiomba kupatiwa huduma ya maji.
Mhandisi Samwel Heche amesema mradi umepokea zaidu ya shilingi milioni mia nane na mkandarasi atakabidhiwa mradi agosti 29,2022 na mradi utakamilika february 2023.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi amewatoa hofu wananchi wa Mkunywa ambapo amesema serikali kupitia Rais Samia Suluhu ina dhamira ya dhati ya kumtua mama ndoo kichwani ndiyo maana imeelekeza fedha nyingi kwenye miradi ya maji.
Aidha Mahundi amesema RUWASA inatekeleza awamu ya pili ya mradi wa maji Lubiga Mawindi ambapo serikali imetoa shilingi 5.2bl ambapo vijiji vitani vitanufaika kupitia mradi huo.
Meneja wa RUWASA Mkoa wa Mbeya Hance Patrick amesema atahakikisha miradi inakamilika kwa wakati.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Reuben Mfune amesema yeye ni jicho la Rais hivyo atahakikisha anaisimamia kikamilifu kama ilivyokusudiwa.
Naibu Waziri wa Maji amepokea taarifa ya utekekelezaji wa miji 28 nchinu ukiwemo mji wa Rujewa ulipata zaidi ya shingili bilioni 29 taarifa iliyosomwa na Meneja wa RUJUWASA Lestus Linda.
Mwakilishi wa Kampuni ya Larren & Toubro Ltd inayotekeleza mradi huo amesema atafanya kazi kwa mujibu wa takwa la mkataba.
Akiwa kijiji cha Ilongo Kata ya Mahongole Diwani Patrick Mwaisoba ameishukuru serikali kwa kutekeleza mradi wa maji Ilongo ambapo wananchi wameanza kupata maji ya bomba.
Akiongea wa viongozi wa Kata ya Mahongole amepiga marufuku wananchi wanaofanya shughuli za kibinadamu katika vyanzo vya maji.
Amesema baadhi ya wananchi wamevamia chanzo cha maji Kongolo Mswiswi na kufanya uharibifu hivyo kuhatarisha ukame katika vyanzo vya maji.
0 Comments