Wakimbiaji Andrew Boniface Rhoby na Winfrida Makenji wanajiandaa kuingia kwenye ngwe za kwanza za mbio zao katika uwanja wa Alexander jijini Birmingham, Uingereza.
Andrew, anayekimbia mita 1,500 ataingia uwanjani saa 5:34 kwa saa za Uingereza ambayo ni sawa na saa 7:34 mchana kwa Tanzania.
Winfrida ataingia uwanjani kukimbia ngwe ya kwanza ya mita 200 saa 5:05 au saa 7:05 ikiwa ni siku tatu baada ya kutolewa
Mashindanoni katika
Mbio za mita 100 kwa matatizo ya kiufundi.
Mwanariadha Andrew, mwenye umri wa miaka 32 na Koplo wa Jeshi la Polisi, atakuwa mmoja wa wakimbiaji watakaokuwa wanajaribu kuvunja rekodi ya mbio hizo za mita 1,500 iliyowekwa miaka 48 iliyopita na Mtanzania Mwenzake, Filbert Bayi, huko Christchurch, New Zealand.
Bayi, ambaye pia yupo Birmingham kama Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) ndiye aliyeteuliwa na waandaaji wa michezo hii ya 22 kutoa medali kwa mshindi wa mbio hizo siku ya fainali yake Jumamosi.
Bayi pia yupo Birmingham kuzindua kitabu cha maisha yake "CATCH ME IF YOU CAN" kinachozungumzia maisha yake. Atakizindua rasmi kesho, siku moja kabla ya mchuano wa mita 1,500.
0 Comments