Header Ads Widget

TANAPA WATOA ELIMU YA UTALII WA NDANI KWA WANANCHI

 


Na Pamela Mollel,Matukio DaimaAPP Arusha 

Shirika la Hifadhi za Taifa Tanapa imejipanga kuongeza idadi ya watalii wa ndani kwa kutoa elimu ya utalii pamoja na kutangaza vivutio mbalimbali vinavyopatikana katika hifadhi zetu kupitia maonyesho ya nane nane


Pia shirika hilo ni miongoni mwa washiriki walioshiriki katika sherehe za nane nane kanda ya kaskazini katika viwanja vya Themi jijini Arusha 


Akizungumza na vyombo vya habari katika banda lao la maonyesho Afisa uhifadhi daraja la kwanza Jerome Boniface alisema kuwa lengo la kushiriki maonyesho hayo ni kuunga mkono  jitihada za Rais kutangaza vivutio na kuhamasisha utalii wa ndani kwa Watanzania 



"Tumeona matokeo makubwa ya Royal tour sasahivi tuna wageni wengi kutoka nje ya nchi wanaokuja kutembelea vivutio vyetu lakini utalii wa ndani bado idadi ni ndogo"alisema Jerome 


Alisema kwa asilimia kubwa wanaokuja katika maonyesho hayo ni wakulima,wajasiriamali wafanyabiashra na watu wengine ambao watapata fursa ya kujua umuhimu wa utalii wa ndani


"Tumebarikiwa sana na Mungu kuwa na vivutio vingi tunawaomba wananchi kutembea vivutio hivyo na gharama yake ni nafuu sanaaa"alisema Jerome 


Aidha alisema kuwa wapo bega kwa bega na Rais Samia Suluhu Hassan hivyo watu wajitokeze katika zoezi la sensa litakalo fanyika August 23 mwaka huu.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI