Header Ads Widget

MLEMAVU ALON AWASHUKURU WALIYOMSAIDIA


Na Amon Mtega, MatukioDaimaAPP

  Songea

MLEMAVU wa viungo (Miguu)Alon Ponera mkazi wa Kitongoji cha Mbwambasi Kijiji cha Mpitimbi Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma amewashukuru wadau mbalimbali zikiwemo taasisi zilizoweza kumsaidia kumpa vitendea kazi ikiwemo pembejeo.


Ponera akitoa shukurani hizo amesema kuwa wadau hao wameweza kumsaidia baada ya kupata taarifa kwenye vyombo vya habari kufuatia kazi za kilimo anazozifanya licha ya ulemavu wake.


Amesema kuwa kufuatia misaada hiyo ameweza kununua mashine za kusaga na kukoboa mbili , Pikipiki moja jambo ambalo linamfanya aendelee kujikwamua kimaisha .



Ponera ambaye amekuwa akifanya za kilimo huku akiwa anatambaa amesema kuwa kazi ya kilimo hawezi kuiacha na anawaomba wadau waendelee kumsaidia ili aweze kufikisha malengo aliyojipangia.


 Aidha katika hatua nyingine amewaomba wadau ambao waliweza kumuahidi kumsaidia zana mbalimbali ikiwemo guta waweze kumsaidia ili aweze kufikisha mazao yake kwa uraihisi zaidi toka shambani,ambapo ameweka mawasiliano yake ya simu,0676-301884.

            Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI