Na Matukio Daima APP Songea,
Wananchi Mkoani Ruvuma wametakiwa kufika katika maonyesho ya nanenane yanayofanyika Uwanja wa Msamala Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma waweze kijifunza teknolojia mbalimbali za ubunifu zilizofanyiwa Utafiti na watafiti katika Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania Tari kituo cha Naliendele.
Akizungumza kwenye uzinduzi wa Maonesho ya Kilimo Nane nane yanayofanyika kimkoa ambapo TARI Naliendele ni miongoni mwa Taasisi zinazoshiriki maonesho hayo mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dkt. Louis Chomboko alisema kuwa hiyo ni fursa muhimu kwa Wakulima na wananchi wa Mkoa huo.
Mwakilishi huyo wa Mkuu wa Mkoa amesifu uwepo TARI Naliendele katika maonesho hayo ambayo yakuws kimekuwa ni kivutio kwa Wakulima katika kujionea teknolojia mbali mbali zilizopo katika banda la kituo hicho hususani teknolojia za mazao kama vile, Korosho, Ufuta, Karanga, Mazao Jamii ya Mikunde, Muhogo na hata bidhaa zitokanazo na uongezaji thamani wa mazao.
"Tunataka Mkulima anufaike na Kilimo chenye tija alime sehemu ndogo apate mavuno mengi kutokana na utaalamu mkubwa walio nao Tari tumeona na tumeshudia teknolojia nyingi kuanzia mbegu hadi uongezaji wa thamani na tunashudia bidhaa nyingi zikitoka kwenye zao la Korosho"
Kwa upande wake Mratibu wa uhaurishaji teknolojia na mahusiano Bakari kidunda alisema kuwa maonyesho hayo ni fursa kubwa kwa watafiti kufikisha teknolojia zao kwa Wakulima Mkoani Ruvuma.
Alisema kuwa ili Kilimo kiwe biashara Mkulima anapaswa kufuata kanuni bora za kilimo na kutumia mbegu bora zilizofanyiwa Utafiti na Taasisi Tari kituo cha Naliendele.
"Ni wajibu wetu kuleta elimu hii kwa Wakulima ili kuongeza tija kwenye Kilimo elimu ambayo itawasaidia kuboresha Kilimo na kuongeza thamani kwa mazao ya Korosho, karanga na Ufuta ambayo tunayafanyia Utafiti kitaifa lakini pia tunafanya Utafiti kwa mazao mengine pia ikiwemo mihogo, VIAZI, mazao ya mbogamboga, kunde,njugu na maharage" alisema Kidunda
"Tunawahamasisha Wakulima kuna kwa wingi kwenye maonyesho ili waweze kijifunza na kujua namna gani wanaweza kupata mbegu bora zilizofanyiwa Utafiti na Taasisi hiyo" alisema Kidunda
0 Comments