Header Ads Widget

MKURUGENZI WA TCB AMEWATAKA WAKULIMA KUENDELEA KUJIFUNZA NAMNA YA KUZALISHA PAMBA YENYE TIJA KATIKA MSIMU WA NANENANE

NA CHAUSIKU SAID, MATUKIODAIMAAPP,MWANZA

Mkurugenzi wa huduma za usimamizi bodi ya pamba Tanzania James Shimbe amewataka wakulima kujitokeza katika msimu wa nanene ili kujifunza namna ya uzalishaji wa pamba yenye tija na kuongeza uzalishaji wa zao hilo.

Hayo ameyabainisha leo katika maonesho ya nanenane na kueleza kuwa wanaendelea kutoa elimu kwa wakulima nchi nzima na kueneza elimu ya kilimo bora cha pamba.

Shimbe amesema kuwa bado wanatoa elimu kwenye uzalishaji wa pamba kwa kutumia vigezo sahihi katika kunyunyuzia viua dudu kwenye shamba na namna ya kutumia vinyunyuzi.


Amefafanua kuwa kutokana na changamoto ya wadudu waitwao chawajane wamekuwa wakivami mashamba na kuharibu mazao wameweza kuwaondoa kwa kushirikiana na watu wa utafiti ukirugulu kwa kuthibiti.

"Viua dudu tumeisha sambaza katika msimu huu na uliopita 2020 hadi 2022 kwa kusambaza viuadudu zaidi ya Mil 9 ili kukabiliana na wadudu wanaoleta usumbufu katika zao hilo" Amesema Shimbe.

Ameeleza kuwa uzalishaji wa zao la pamba unaweza kuwa wa juu au ukashuka hivyo husababishwa na mabadiliko ya tabianchi.

Shimbe amesema kuwa malengo ni kuwafikia wakulima zaidi ya mikoa 17 ambayo ipo kwa sasa na kuendelea kufikia mingine yenye ardhi nzuri kwa kilimo cha pamba


Ameeleza kuwa uzalishaji wa msimu uliopita ulikuwa wa tofauti wa tani 148000 huku tani tani 150000 uzalishaji huo ulikuwa wa juu kidogo ya msimu uliopita ambao ulikuwa ni tani 124000 ambapo ongezeko hilo limechangiwa na utoaji wa elimu kwa wakulima kwa kupitia balozi wa zao hilo.

"Na ikumbukwe kwamba hapo nyuma tulikuwa na utaratibu wa uzalishaji kwa kupanda miche 2222 kwa tani 1 kwa sasa kumekuwa na mabadiliko unapanda miche 4444 kwa tani 1 unapata mara mbili ya uzalishaji wa mwanzo.


Amesema kuwa uzalishaji umeongezeka zaidi mara mbili ya hapo kwa maana ya mwanzo wakulima walikuwa wanalima miche michache kwa sasa wanalima kilimo cha kisasa kwa kufata kanuni na vipimo vipya hivyo mazai kuongezeka.

Aidha amewataka wanachi kufika ili waweze kujifunza na kuona mchakato wa mbegu unavyofanyika hadi kufikia hatua ya kurudishwa shambani.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI