

Baadhi ya wanachama wa Kigoma Press klabu wakiwa katika picha ya pamoja na ujumbe kutoka baraza la habari Tanzania(MCT)baada ya kutembelea hizo za klabu hiyo
***********************
Na Editha Karlo,Kigoma
Mkurugenzi mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania- (MCT) Kajubi Mkajanga amewataka waandishi wa habari kuyatumia machapisho yanayotolewa na MCT katika kujifunza mambo mbali mbali yaliyoandikwa ndani ya vitabu hivyo.
Ameyasema hayo kwenye ziara ya kutembele ofisi ya Kigoma Press Club,wakati akikabidhi machapisho kwa mwenyekiti wa chama cha waandishi wa Habari Mkoa wa Kigoma -(KGPC) Deogratius Nsokolo kwaajili ya klabu hiyo,baada ya kumaliza mafunzo habari za uchunguzi ya siku 4 kwa waandishi wa habari wanawake Tanzania.
Alisema machapisho anayokabidhi ni pamoja na kanuni za maadili ya unadishi wa habari toleo la mwaka 2020, mwongozo wa vyombo vya habari wa kuandikahabari za watoto, mwongozo wa kupata na kutoa taarifa kwa waandishi wa habari na maafisa habari na mwongozo wa wakufunzi katika uandishi wa data na jinsia.
Alisema, MCT inaendelea kufanya kazi na Press Club zote nchini lengo ikiwa ni kuimalisha mahusiano yaliyopo kati Baraza la habari Tanzania- (MCT) na Muungano wa Press Club Tanzania -(UTPC).
Naye Rais umoja wa klabu za waandishi wa habari Tanzania(UTPC)Deogratius Nsokolo alisema utpc itaendekea kushirikina na baraza la habari Tanzania(MCT)pamoja na taasisi nyingine za habari ili kuboresha mahusiano na kufanya kazi kwa pamoja.
Nsokolo alishukuru baraza la habari kwa kupatia kigoma press Club vitabu mbalimba vya taalum,miongozo na machapisho ili wanachama waweze kujifunza mambo mbalimbali.
0 Comments