Header Ads Widget

MARUFUKU MAKARANI KUPIGA PICHA NA KUREKODI MAHOJIANO WAKATI WA ZOEZI LA SENSA LIKIENDELEA

 

Mtakwimu Mkuu wa Serikali wa Sensa ya Watu na Makazi Dr. Albina Chuwa amewaonya Makarani wa sensa Kuacha kupiga Picha na kurekodi Mahojiano pindi wakiwa kwenye Kaya za watu  na kuyaifadhi ama  kuyachapisha Mitandaoni kwani kwa kufanya hivyo ni kosa la Jinai na linakiuka na kwenda Kinyume na kanuni, Sheria na Maelekezo na atakayebainika adhabu yake ni kifungo Jera miezi sita au Faini ya Milioni 2 au vyote kwa Pamoja. 



"Makarani wa Sensa Nchi nzima, tunavyokwenda kwenye kaya za watu tuache kupiga picha, tuache kurekodi watu ni kosa la Jinai, kwani taarifa hizi mlizoambiwa mkazichukue ni za siri kufanya hivyo makarani wa sensa na sasa hivi tumeshashika kesi na zipo kwenye Vyombo vya kisheria na hatua zinachukua Mkondo wake"


Pia amewasihi wakazi wa Iringa Kuendelea Kujitokeza Kuhesabiwa na kutoa taarifa Sahihi.


Aidha Dk. Albina Chuwa amesema kuwa kwa Mkoa wa Iringa zoezi la Sensa ya watu na makazi linaendelea Vizuri kwa ufanisi mkubwa kwani Mpaka sasa Asilimia 80 (80%) ya watu tayari wamehesabiwa. 


Zoezi alilofanya katika ziara hii ni kupita Kaya kwa Kaya ili kujilizisha juu ya usahii wa taarifa zinazotolewa na wanakaya na zile zinazorekodiwa na Makarani, alifanya hivyo kwa kuwaoji baadhi ya wanakaya na kuangalia taarifa kwenye Kishikwambi cha Karani kama Zinaendana. 

Zaidi akawataka wasimamizi wa zoezi la sensa katika maeneo husika kufanya ukaguzi kama alivyofanya yeye. 

Ameyasema yote haya akiwa Mkoani Iringa katika Ukaguzi wa Zoezi la Sensa ya Watu na Makazi.


















Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI