Na HADIJA OMARY _LINDI
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Lindi imeendelea kusogeza mbele kesi ya mauwaji inayowakabili Maofisa watatu wa Magereza Mkoani Lindi akiwemo Mkuu wa Gereza la Liwale Mkoani humo SP Gilbert Sindani na kupangwa kusikilizwa tena Augost 15 mwaka huu kutokana na ushahidi wa kesi hiyo kuto kamilika
Hii ni mara ya nne kwa watuhumiwa hao kufikishwa Mahakamani hapo ambapo kwa mara ya kwanza walifikishwa Mahakani juni 23 ,2022 na leo wamefikishwa Mahakamani na kesi yao kuhailishwa mpaka August 15 mwaka huu huku watuhumiwa wa kesi hiyo wakilazimika kusalia rumande
Watuhumiwa wengine wa kesi hiyo ni pamoja na Sajent yusuph Athumani na Coplo Fadhili Afwad wote ni maofisa wa gereza la Liwale
Kesi hiyo yenye namba RMPI 1 ya mwaka 2022 iko chini ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa wa Lindi Consolatha Singano imesikilizwa kwa mfumo wa kimtandao ambapo baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Mwanasheria wa Serikali kuwa upelelezi wa kesi hiyo ya Mauaji kutokamilika ndipo akaipangia tarehe nyingine ya kusikilizwa.
0 Comments