WANAOSAKA UBUNGE 2025 WAKEMEWA VIKALI - Matukio Daima-Mzee wa matukio

Latest

MAGAZETI

imageedit-1-7612421179
imageedit-1-4504100673
imageedit-3-3876648809

Latest news! +255 754026299! Latest news! matukiodaima3@gmail.com!

Wednesday, July 13, 2022

WANAOSAKA UBUNGE 2025 WAKEMEWA VIKALI

 


Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Daniel Chongolo amekemea tabia ya baadhi ya wanachama kuanza kujipitisha katika majimbo kutafuta wapambe ili wawasaidia kwenye malengo yao ya Ubunge na udiwani kwa mwaka 2025.


Katibu Mkuu ameeleza kuwa, Chama hakitasita kuchukua hatua kwa mujibu wa taratibu, kanuni na katiba ya CCM ili kuwadhibiti watu hao, kwani muda wa uchaguzi bado na sasa kila jimbo lina mbunge na kila kata kuna diwani hivyo ni vema kwa kila mwanachama kusubiri muda ufike na sio kuanza sasa wakati viongozi waliochaguliwa wanafanya kazi ya kutekeleza Ilani ya Uchaguzi.


Katibu Mkuu Chongolo ameyasema hayo leo tarehe 13 Julai, 2022 wakati akifungua kongamano la Mafunzo ya Uongozi kwa mabalozi wa mashina na viongozi wa matawi mkoa wa Dodoma .No comments:

Post a Comment

Habari za kitaifa! Habari ya Kimataifa! Habari za Michezo/Burudani !