Header Ads Widget

WANANCHI NJOMBE WASHAURIWA KUENDELEA KUJITOKEZA KUCHANJA CHANJO YA UVIKO-19

 



Na Gabriel Kilamlya NJOMBE


Wananchi mkoani Njombe wamesisitizwa kujitokeza kuendelea kupata Chanjo ya UVICO 19 ili kuimarisha kinga za miili yao kwani ugonjwa wa Corona bado ungali.


Katika mikutano ya hadhara ya mkuu wa wilaya ya Njombe  Kissa Kasongwa katika mitaa mbalimbali mjini Njombe wakazi hao wamekumbushwa kuendelea kupata chanjo hiyo ambayo imekuwa msaada mkubwa katika kukabiliana na ugonjwa huo pindi unapomkuta mtu.


Akiwa katika mtaa wa Idundilanga mjini Njombe Mkuu huyo wa wilaya   amesema ni muhimu kupata chanjo hiyo kwani ugonjwa ukimkuta mtu humsababishia hasara kubwa na wakati mwingine kifo kwani kinga ni bora kuliko tiba.


Baadhi ya wakazi wa Njombe mjini akiwemo Anjela Mwangeni na Deodata Mlowe Wamekiri Kuwa Wamechanja na Hakuna Madhara Waliyoyapata na Kwamba ambao hawajapatiwa wanapaswa kuendelea kupata Chanjo hiyo.



Abdalah Liku,Andreas Mahali na Nassoro Hamidu ni Vijana ambao wamejitokeza mbele ya mkuu wa wilaya ya Njombe na kukiri kuwa Chanjo imezidi kuwaimarisha katika familia zao.


Serikali imeanza tena kutoa chanjo ya Covid 19 aina ya Johnson and Johnson ambayo inatolewa mara moja.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS