Header Ads Widget

*DKT SAMIA: TANZANIA ITAVUKA NA KUSONGA MBELE*


Waziri Mkuu wa Tanzania, Dkt Mwigulu Nchemba amesema Serikali haitakuwa kikwazo cha kuhakikisha nchi inakuwa moja na inasonga mbele, baada ya kupita katika changamoto.

Akizungumza kwa niaba ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, mtendaji mkuu huyo wa Serikali, amesisitiza tayari kuna utashi wa kisiasa wa kujenga umoja nchini na kwamba jukumu hilo amekabidhiwa yeye.

Dkt Nchemba ametoa kauli hiyo jijini Arusha leo, Jumamosi Januari 24, 2026 alipotoa salamu za Serikali kwa Rais Dkt Samia, aliyemwakilisha katika maziko ya Gavana wa kwanza wa Tanzania, Edwin Mtei.

“Serikali haitakuwa kikwazo cha kuhakikisha kwamba nchi inakuwa moja na tunasonga mbele na mimi niwahakikishie tutavuka na tutasonga mbele na heshima ya Tanzania ya mara zote tutakuwa nayo,” amesema.

Amesema Rais Dkt Samia angependa kushiriki maziko hayo, lakini wingi wa majukumu umemfanya amtume yeye kumwakilisha na kwamba yaliyozungumzwa na wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini ameyachukua.


 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI