Header Ads Widget

WAANDISHI WA HABARI KIGOMA WAFANYA MDAHALO NA JESHI LA POLISI

 


Makamu Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari Mkoa wa Kigoma(KGPC)Jacob Ruvilo akichangia mada wakati wa mdahalo wa ulinzi na usalama kati ya waandishi wa habari wa Mko wa Kigoma na jeshi la polisi

Na Editha Karlo, MatukioDaimaAPP,Kigoma

KLABU ya waandishi wa habari Mkoa wa Kigoma(KGPC)imeendesha mdahalo wa ulinzi na usalama kwa waandishi wa habari Mkoani humo huku lengo la mdahalo huo ni kufanya kazi kwa kushirikiana baina ya jeshi la polisi na waandishi wa habari.


Mdahalo huo ambao umeandaliwa na KGPC chini ya ufadhili wa umoja wa klabu za waandishi wa habari Tanzania(UTPC) ikishirikiana n shirik la International Media Support(IMS).


Akizungumza wakati akifungua mdahalo huo kwa niaba ya Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Kigoma Ramadhani Kingai,Filemon Makungu ACP alisema kuwa kuwepo kwa mdahalo huo ni moja ya kuwa na lengo jema katika maisha ya waandishi wa habari na polisi Mkoani humo.



‘’Sisi sote tunafanya kazi zetu kwa mujibu wa sheria,hivyo kila mmoja anawajibu wa kulinda haki ya kila mmoja kiutendaji bila upande wowote kuathirika,tufanye kazi kwa kushirikiana huku tukiweka maslahi ya Taifa mbele’’Alisema


Aliwataka waandishi wa habari Mkoani humo kufuata maadili ya kazi yao na kuepuka kufanya habari au kupiga picha ambazo hazina maadili au utu pia ili kazi ziwe nzuri wanahabari wanapaswa kufanya kazi  weledi na kuandika habari ambazo ni sahihi na siyo kuandika habari za kuleta taharuki katika jamii.


Makungu aliwataka waandishinwa habari kuendeleza ushirikiano mzuri walionao na jeshi la polisi pia alitaka midahalo kama hiyo iwe ni endelevu.


Naye Makamu Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari Mkoa wa Kigoma(KGPC)Jacob Ruvilo alisema kuwa waandishi wa habari na jeshi la polisi wanapaswa kuwa na mahusiano mazuri,kwasababu kazi zao zinategemeana hasa kwenye matukio ya kiharifu na ajali za barabarani.


‘’Lengo la kuwa na mdahalo huu ni kuboresha mahusiano kati ya jeshi la polisi na waandishi wa habari hasa katika utekelezaji wa majukumu yetu’’alisema Ruvilo


Ruvilo aliwataka wanahabari kufanya kazi ya kuhabarisha umma kwa kufuata maadili ya kazi zao na kuheshimiana.


‘’Sasa hivi mambo ya utandawazi yameshika kasi hali inayofanya sasa hivi unakuta kila mtu anajikuta ni mwandishi wa habari hivyo tunapaswa kuheshimiana kwa nafasi zetu kwa maana ya polisi na wanahabari”alisema Makamu Mwenyekiti wa KGPC


Alisema waandishi wa Mkoa wa Kigoma wapo tayari kushirikiana na Jeshi la polisi katika kutekeleza majukumu ya kujenga Taifa huku wakizingatia taratibu za kazi zao.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI