Header Ads Widget

RC, MWANZA ATOA NENO KWA WADAU WALIOTOA MSAADA BAADA YA BWENI LA BWIRU BOYS KUUNGUA NA MOTO.




NA CHAUSIKU SAID, MWANZA.


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel amewashukru wadau mbalimblai waliojitokeza kutoa misaada baada ya bweni la shule ya wavulana bwiru boys kuungua kwa moto.


Ameyaeleza hayo wakati akipokea misaada ya sabuni,  mafuta pamoja na viatu vya shule kutoka Benk ya CRDB  pamoja na chuo cha DIT.



Gabriel amesema kuwa amekuwa akipokea misaada kutoka kwa wadau mbalimbali ambao wamewaunga mkono ili kuhakikisha wanafunzi waliopatwa na janga la kuunguliwa na vitu vyao wanapata misaada itakayowasaidia kurudi katika hali ya zamani.


"Tumeona wengi wakileta misaada hapa shuleni na lei tumepokea sabuni,  mafuta,  pamoja na viatua, lakini mbali na  changamoto hizi tunazozipata Mwanza tunaona kuna watu wengi wanatuunga mkono katika matukio mbalimbali ya kimaendeleo pamoja na kijamii" Alisema Gabriel.


Hata hivyo amefafanua kuwa baada ya bweni hilo kuungua moto watalamu wamepitia mabweni yote pamoja na jipya linalojengwa ili kuhakikisha hakuna nafasi ya mwanafunzi kupita juu ya silingibodi kwa ajili ya kufanya mabadiliko yoyote ya nyaya yanafanyika.


" Tumehakikisha tunaweka ulinzi wa kutosha kwa jengo jipya linalojengwa ndani na nje pamoja na mabweni mengine yote kujidhilisha hakuna vitendo viovu vinajitokeza.



Amesema kuwa wataongeza ulinzi katika mabweni ili kuhakikisha hakuna majanga mengine yatakayoweza kujitokeza na kuweka miundombinu rafiki kwa wanafunzi.


Aidha amewataka wazazi wa wanafunzi waliopata majanga ya moto kuwa na amani kwani hali ya watoto wao imeimalika na vifaa walivyokuwa wanahitaji tayari wamepata.


Joyce Maruba ni Meneja Mahusiano Benk ya CRDB kanda ya ziwa amesema kuwa wamekuwa wakitoa misaada mbalimbali kwa wanafunzi hao tangu kuungua kwa bweni hilo ili waweze kupata mahitaji muhimu kwa ajili ya matumizi yao binafsi wawapo shuleni.



" kama benk ya watanznia, serikali tumekuja kuwasaidia kuwapa mahitaji yatakayoweza kuwasaidia lakini pia hawa ni watoto wetu Benk ya CRDB inawathamini sana na kuwependa na ndio maana tuko hapa kwa ajili ya kuwapa misada baada ya janga la moto" Alisema Joyce.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Chuo cha DIT Dr Albert Mmari amesema kuwa walipopata taarifa hizo za changamoto ya kuungua kwa moto bweni la wavulana shule ya bwiru boys wakaamua kutoa msaada wa viatu kwa wanafunzi hao.



" Tukasema sisi tukiwa kama Taasisi ya serikali ni lazima tuje tuunnge mkono serikali yetu kwa kutoa viatu ili mhakikishe mnakuwa na sale kamili ya shule" Alisema Mamri.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI