Header Ads Widget

VITENDO VYA MAUAJI ,UBAKAJI NA ULAWITI NJOMBE VISIPEWE NAFASI

 


Na Frederick Siwale - Mdtv Media - Njombe.       


WITO umetolewa kwa Jamii kupiga vita vitendo vya ukatili wa kijinsia vikiwepo vya Mauaji, Kishirikina ,Ubakaji na Ulawiti ili kuleta amani na utulivu kwa Wananchi Mkoani Njombe.                               


Rai hiyo imetolewa na Bi.Apia Mayemba aliyekuwa mgeni rasmi katika ufungaji atwa mafunzo ya umoja wa amani kwanza yalifanyika kwa muda wa siku mbili ya kuwajengea uwezo Wanachama wa (UAK) yaliyofanyika katika ukumbi wa Polisi Wilaya ya Kipolisi Makambako.                     


Bi.Mayemba ambaye alikuwa amemwakilisha Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Mji Makambako , Bw.Keneth Haule alikuwa  mgeni rasmi akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Njombe ,Bw Waziri Kindamba ambaye alikuwa ndiyo awe mgeni rasmi ila kutokana na sababu zilizokuwa nje ya UAK Mkoa .                                



"Nipende kutoa pongezi kwa Raisi wa Taasisi ya Umoja wa amani kwanza Dr.Wilson George kwa kuanzisha taasisi hii ya umoja wa amani kwanza maana utakuwa mkombozi kwa Jamii ya Wananjombe." Alisema bi.Mayemba.       


Mkoa una matarajio chanya kutoka kwenu Wana Umoja wa amani kwanza iwapo mtatenda kazi kwa weledi na uadilifu mkubwa alisema Bi.Mayemba katika hotuba yake.                       



Awali akifungua mafunzo ya uzalendo kwa Wanachama 32 wa Umoja wa amani kwanza mkoani Njombe Mkuu wa Upelelezi  ( OC - CID) Wilaya  ya kipolisi Makambako  Afande ASP. Josam Gabikwa  aliwataka Wana Umoja wa amani kwanza kwenda kuwa mabalozi wazuri na kuitumia vyema elimu waliyoupata kutoka kwa Wawezeshaji wa vyombo vya ulinzi na usalama  Mkoa wa Njombe .                              



"Hakikisheni elimu hii mliyoipata inaleta  tija kwa Wananchi huko mtakakokuwa mnatoa elimu na kutolea taarifa kwa Jeshi la Polisi ili kudumisha amani na kukomesha vitendo vyote vya uhalifu" Alisema ASP Gabikwa.                                 


Upande wake Rais wa Taasisi ya umoja wa amani kwanza (U.A.K) Dr.Wilson George aliwafunda Wanachama hao kuepuka kwenda kuwa wavunja amani kwa kugeuka waomba rushwa au kujiita Polisi badala ya kujiita Wasaidizi wa Vyombo vya ulinzi na usalama . 



" Nitashangaa sana kusikia mmoja wenu kati yenu ninyi mliopata mafunzo nitasikie eti yupo mahabusu amekamatwa kwa kujihusisha na mambo ya hovyo na kwa taarifa yenu Polisi hawa kuwageuka ni sekunde,kafanyeni kazi ya kutoa taarifa kwenye Mamlaka na hasa vyombo vya ulinzi na usalama na hasa Polisi." Alisema Dr.Wilson George.             


Aidha Wawezeshaji wa mafunzo Mkaguzi msaidizi wa Polisi Donard Moses Mkuu wa Interejensia Wilaya ya Kipolisi Makambako, Mkuu wa kituo cha Polisi Tazara Makambako ,Mkaguzi msaidizi wa Polisi Balele Lutema na Inspekita Curhbert Mlaponi Kasembe Mfawidhi kituo cha Uhamiaji Makambako katika mada tofauti walisisitiza amani na uzalendo ili kulinda amani kwa Wananchi ikiwa ni pamoja na kutolea taarifa vitendo vyote vya kihalifu ikiwa ni pamoja na uingiaji Wahamiaji haramu katika maeneo yao.                     



Wakufunzi wengine walioshiriki kutoa elimu katika mafunzo hayo ni afisa mikopo wa benki ya CRDB tawi la Makambako Bi.Mwajuma Mwalemba, Francis Ngatunga kutoka dawati la  jinsia Wilaya ya Kipolisi Makambako .                     


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI