Header Ads Widget

UJENZI WA BARABARA ZA MAWE ZAWAINUA WANAWAKE KIUCHUMI.

Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Barabara Octavian Mshiu akimuelekeza jambo Meneja wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) Mhandisi Goodluck Mbanga (wa kwanza kulia)
Meneja Tarura Mkoa wa Mwanza


**********************

NA CHAUSIKU SAID, MWANZA.

Ujenzi wa Barabara mbalimbali za mawe Mkoani Mwanza zawainua wanawake kiuchumi Kwa kupata ajira ya uchongaji mawe na ujenzi kwa ujumla.

Hayo yamebainishwa na baadhi ya wanawake wanaofanya kazi hiyo wakati wa Ziara ya Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Barabara Octavian Mshiu akiwa na wajumbe walipotembelea miradi ya barabara zinazojengwa kwa mawe.

Monica Mawi na Iren Mussa ni miongoni mwa wanawake wanaofanya kazi ya upondaji mawe wamesema kuwa ajira hiyo imewasaidia kujikwamua kimaisha, kuwapeleka watoto shule pamoja na kutengeneza miundombinu ya nyumba wanazoishi.

" kiukweli kazi hii ya uchongaji mawe imetusaidia kwa kiasi kikubwa katika maisha hususani kwenye ujenzi ijapokuwa nyumba aijakamilika vizuri lakini angalau" Walisema.

Mshiu amesema kuwa kutokana na Rais Samia kuhimiza swala la ajira kwa wazawa Bodi ya mfuko wa Barabara imetoa fedha zitokanazo na tozo mbalimbali kwa ajili ya kusaidia miradi ya Barabara inayosimamiwa na Tanroad, Tarura pamoja na kushughulika kwa ajili ya ujenzi wa barabara za mawe na zimeweza kutoa ajira kwa wanawake na vijana jiji hapa.

"Tumeenda sehemu ambayo ni mgodi wa kuandalia mawe tukaona maajabu kwa sababu eneo lile limeajili vijana wengi lakini tukaona kuna vijana kuanzia umri wa 18 wa kike kwa kiume wanafanya kazi, kumbe kungekuwa na vijana wengi wanashinda mitaani, majumbani wakisema serikali.haijawapa ajira, lakini vijana wa mwanza tumewakuta wanachonga mawe na kipato kwa siku ni sh. Elfu 30 hadi 60.

Meneja TARURA Mkoa wa Mwanza Goodluck Mbanga,ameeleza kuwa ujenzi wa barabara za mawe mkoani Mwanza umeokoa fedha nyingi ambazo serikali imekuwa ikitumia katika kurudia matengenezo katika barabara za gravu pamoja na kutoa ajira kwa wazawa.

"Kwa kifupi inatusaidia sana kwa sababu Jiji la Mwanza lina miinuko na miinuko yenye mawe na kwenye miinuko barabara hizi za gravu zinashindwa kuhimili na magari yanashindwa kupandisha kwa sababu mvua zikinyesha muunganiko wa mawe na gravu unakuwa siyo mzuri,", ameeleza Mbanga.

Mbanga ameeleza kuwa Jiji la Mwanza kwa maana ya Wilaya ya Nyamagana na Ilemela wana zaidi ya Km 2000 za barabara huku za mawe ni km 16.

"Ni chache sana asilimia kubwa ya barabara zetu ni udongo tunahitaji sana barabara za mawe kwa kiasi kikubwa tulichofanya ni kama tone sawa na asilimia 0.2, tunashukuru bkuoata vyanzo vya fedha kwa kumalizia barabara hizi ambazo nyinginzipo katika hali siyo nzuri,"ameeleza Mbanga.

Kwa upande wake Mhandisi wa barabara Wilaya ya Nyamagana Jane Mdula, ameeleza kuwa utekelezaji wa ujenzi wa barabara za mawe kwa asilimia kubwa inafanywa na watu na siyo mitambo.

Mhandisi Jane ameeleza kuwa gharama za ujenzi wa barabara za mawe ni nafuu kidogo ukilinganisha na nyingine mfano barabara hiyo ambayo Ina urefu wa mita 370 na gharama yake ni milioni 167.

",Kwa hiyo tunatengeneza ajira kwa watu wanaochonga mawe ya kujenga barabara ambayo yanachongwa kwa mkono pia ujenzi wake ni WA gharama nafuu ukilinganisha na ujenzi wa barabara zingine" Alisema Jane.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS