Header Ads Widget

RAIS SAMIA KUWA MGENI RASMI SHEREHE ZA MASHUJAA DODOMA

 


Na Hamida Ramadhan Matukio Daima App Dodoma

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Sherehe za mashujaa ambayo kitaifa itafanyika tarehe Julay 25 jijini Dodoma


Akizungumza katika viwanja vya Mashujaa ambapo Sherehe hizo zitafanyika Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka alisema kuwa maandalizi yanaenda vizuri na kamati ya Ulinzi na usalama imeridhishwa na maandalizi hayo.


Mtaka alisema kuwa tarehe 24 usiku saa sita kamili uongozi wa mkoa na viongozi mbalimbali watakuwa katika viwanja hivyo kwaajili la zoezi la kuuwasha mwenge kuamkia siku ya mashujaa kitaifa na siku ya tarehe 25 ambayo ndio siku ya mashujaa usiku saa sita kamili mwenge huo utazimwa katika viwanja hivyo.



Aidha alisema kuwa wako tayari kuhakikisha eneo hilo la mashujaa linakuwa hai kama ambavyo maeneo kama hayo kwenye maeneo mengine duniani yanavyotumika.


"Rais Samia amewapa heshima kubwa sana wakazi wa mkoa wa Dodoma kwani ipo mikoa mingi yenye minara ya mashujaa lakini imempendeza Mheshimiwa Rais shughuli hii kitaifa iweze kuwafanyika hapa,"alisema Mtaka.


Na kuongeza "Kwetu sisi mnara wa kumbukumbu za mashujaa wetu ndani ya Jiji la Dodoma tutautunza lakini tunatamani liwe ni eneo ambalo litatembelewa,liwe ni eneo ambalo litakuwa ni moja ya alama za mkoa wa Dodoma na ni moja ya eneo la kuvutia watu kwasababu ni eneo lipo kwenye eneo zuri na linaonekana na linafikika kwaiyo Ofisi ya mkoa,ofisi ya Jiji la Dodoma na Ofisi ya maadhimisho tutakutana pamoja tukubaliane namna gani eneo hili litatunzwa vizuri," alisema Mtaka.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa maadhimisho Taifa Ofisi ya Waziri Mkuu Bathilomeo Jungu alisema kuwa maandalizi yanakwenda vizuri Kutokana na kuwa eneo hilo halikuwa zuri lilikuwa limechoka na kazi ya ukarabati wamewakabidhi SumaJkt ili kuhakikisha eneo hilo linakarabatiwa na kuwa katika hali nzuri

Sherehe za mashujaa kitaifa kwa mwaka 2022 zinafanyika Dodoma na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atakuwa mgeni rasmi kwenye siku ya mashujaa kitaifa tarehe 25/7 ambayo itakuwa siku ya jumatatu na shughuli zitaanza asubuhi mapema.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI