Header Ads Widget

MWENYEKITI BODI YA MFUKO WA BARABARA AKAGUA DARAJA LA JPM ATOA NENO



NA CHAUSIKU SAID , MATUKIODAIMAAPP,MWANZA

Menyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Barabara Joseph Haule ametembelea daraja la JPM linalounganisha wananchi wa Kigongo feli na Busisi Mkoani Mwanza na kuona namna ujenzi huo unavyoendelea.

Haule amesema kuwa lengo la kufanya  ziara hiyo ni kufahamu teknolojia iliyotumika  pamoja na kujilidhisha ujenzi unavyoendelea,  pindi watakavyokabidhiwa daraja hilo wawe wamekabidhiwa kitu kilichokamilika na ambacho kitadumu kwa muda mrefu.

Amefafanua kuwa daraja hilo lenye urefu wa kilometa 3.2 ambalo litadumu kwa muda wa miaka 100, pia litakuwa la sita Afrika na litakabidhiwa ifikapo 24 April 2024 kwa serikali.


"Kwa kweli kama mnavyoona Tanzania inazidi kupaa tumeona madaraja mengine yamekuja kuchukua rekodi lakini hili ndio litavunja rekodi nchi za  Afrika Mashariki na kati" Alisema Haule.

Aidha amesema kuwa mbali na uwepo wa changamoto za Uviko, maji kuongezeka,  pamoja na uwepo wa miamba lakini watalamu wamezingatia ubora katika ujenzi utakaosaidia kupata daraja bora ambalo halitaharibika mapema.

Meneja Msaidizi wa Bodi ya Mfuko wa Barabara Mhandisi Rashidi  kalimbaga amesema kuwa kazi kubwa ya Bodi hiyo ni kukusanya fedha itakayosaidia kufanya matengenezo ya barabara na madaraja yote Tanzania Bara zinazohusika na Tanroad pamoja na Tarura.

Kalimbaga amesema kuwa Madaraja yote yakishatengenezwa Bodi ya Mfuko wa Barabara wanawajibu wa kuhakikisha yanakuwa kwenye ubora wake ili yaweze kutumika kwa muda uliopangwa

" kama hili daraja la miaka 100 lazima tujakikishe linapata matengenezo ili liweze kuishi kwa kipindi cha miaka 100 na kama ni barabara tunafanya hivyo hivyo ili kuhakikisha tunapeleka fedha kwa Tanroad na Tarura" Alisema Kalimbaga.

Nae Meneja wa Tanroad Mhandisi Pascal Ambrose amesema kuwa ujenzi wa daraja hilo unakwenda kama ulivyopanga pia ameeleza kuwa watanzania bado wanauelewa mdogo juu ya utunzaji wa mali za serikali.

" wengi hatuelewi kwamba hizi mali za serikali ni mali zetu wenyewe mtu anadiliki kuiba kitu kwa lengo la kujipatia mkate wa siku moja hakumbuki madhara yanayotokea  ni mkubwa na kirudisha maendeleo nyuma na kubaki jambo moja linafanywa kwa muda mrefu" Alisema Ambrose.

Ambrose amesema kuwa watanzania kujifunza kutunza mali za umma kwani ni mali zao zitakazowasaidia mbeleni na kuacha kiwarudisha nyuma kwa  kufanya kazi mara mbili mbili.

Kwa upande wake Mhandisi Mshauri  Abdukarim Majuto ameeleza kuwa mradi umefikia Asilimia 48.97 na mpaka sasa nguzo 22 kati ya 67 ziko tayari zimeishainuliwa na kulaza nguzo ulalo

Aidha Majuto amefafanua changamoto ya wizi uliokuwepo hapo awali limeweza kuimalika baada ya kamati ya ulinzi na uslama kutembelea daraja hilo .



" Tangu kuundwa kwa kamati ya ulinzi na usalama imekuwa inatembelea eneo hili kila wakati iwe mchana au usiku kwa njia ya maji na nchi kavu pia mkandarasi ameanza kuweka kamera zitakazobaini watu wanoiba" Alisema Majuto.





Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI