Header Ads Widget

TAMASHA LA MZIKI MNENE KUHAMASISHA CHANJO YA UVICO19

 

NA MATUKIO DAIMAAPP,MTWARA

 Mtwara, Tamasha la mziki mnene linalotarajiwa kufanyika mkoani mtwara katika viwanja vya nangwanda Julai 23 ambapo litahudhuliwa na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu sambamba na utolewaji wa chanjo ya UVICO19 na kuongozwa na Msanii Hamonise. 


Katika tamasha hilo watu zaidi ya 20,000 wanatarajia kuchanjwa ambapo tamasha hilo litafanyika katika wilaya zote za mkoa huo wakiwa na lengo la kuhamasisha wananchi kujitokeza. 


Akizungumza na waandishi Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Brigedia Generali Marco Gaguti alisema kuwa wananchi wajitokeze.  

Alisema kuwa tamasha hilo litasheheni wasanii mbalimbali wakiongozwa na hamonise kwaajili ya kuhamasisha uchanjaji wa chanjo ya UVICO19. 


“Tumeona ipo haja ya kuhamasisha uchanjaji wa chanjo hii ili kuwa na taifa lenye uhakika na kinga ya kutosha hali ambayo itaongeza hamasa ya kufanya shughuli za maendeleo kwa nguvu zaidi na tutaongeze idadi ya ulinzi wa afya zetu”


Nae Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Hamad Nyembea alisema katika tamasha hilo zaidi ya wananchi 100,000 watachanjwa chanjo ya UVICO19 ndani ya siku 10.


Wapo watu waliojitokeza awali wakachomwa chanjo ya JJ hao hawana shida lakini wapo waliojitokeza wakachanja hii ya pili na wamechomwa moja pia ya kurudia itakuwepo ni vema wakajitokeza na kujitoa kwani ulinzi wa afya yako unaanza na wewe mwenyewe”

“Tunarajia kuwa na asilimia 70 ya wananchi walipata chanjo ya UVICO9 hii itasaidia kupunguza kasi ya maambukizi ya ugonjwa huo ambapo wote waliochanja wako salama” alisema Dr Nyembea



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI