Header Ads Widget

OJADACT YAFANYA MAADHIMISHO YA SIKU KUPIGA VITA MATUMIZI YA DAWA YA KULEVYA NA UHALIFU TANZANIA.

 

NA CHAUSIKU SAID,MATUKIO DAIMAAPP,MWANZA

CHAMA  cha waandishi wa habari wa kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya na uhalifu (OJADACT) Mkoa wa Mwanza kimefanya maadhimisho hayo kwa lengo la kuendelea kuelimisha jamii ili kuepukana na matumizi mabaya ya dawa za kulevya.




 Edwin Soko ni mwenyekiti wa chama hicho amesema kuwa maadhimisho hayo hufanyika kila mwaka ili kuendelea kutoa elimu itakayowezesha jamii kufahamu athari za madawa ya kulevya.



Ameongeza kuwa Waandishi wa habari wanapaswa kuelimisha jamii kwa kuandika habari zitakazofanya jamii isitumie dawa za kulevya ambazo zina athari katika jamii,kielimu pamoja na kiuchumi hali itakayopelekea kupungua kwa matumizi ya dawa hizo.



"Na hapa nasisitiza dawa za kulevya hazina afya kwa jamii, dawa za kulevya ni nguzo mbaya Sana za mmomonyoko wa maadili na mstakabali wa maisha na umoja katika familia kwani Kuna athari kubwa katika kutumia dawa hizo"amesema Soko. 


Kwa upande wake Mganga Mkuu wa hospitali ya Rufaa sekoutoure Dr Thomas Rutachunzibwa amesema kuwa Wazazi na walezi mkoani mwanza  wameshauriwa kufatilia mienendo ya watoto wao katika ngazi ya familia ili kuhakikisha makuzi na tabia zinakuwa za kimaadili.



Dr Rutachunzibwa amesema kuwa wazazi na familia kwa ujumla kuhakikisha watoto wao wanaenenda katika maadili mema hali ambayo itasaidia kupunguza idadi ya vijana wanaotumia dawa za kulevya.



"Familia ndio msingi mkubwa wa kuhakikisha kwamba tunathibiti matumizi ya dawa za kulevya katika jamii Zetu tukiwalea vizuri watoto wetu ukawafatilia tutakuwa tumewaepusha na hili janga la dawa za kulevya"amesema Dr Rutachunzibwa.



Ameongeza kuwa dawa za kulevya zinaathiri akili na ubongo vinakuwa katika  hali ya tofauti hali inayopelekea mraibu kufanya kitu chochote bila ya aibu.



Akizungumzia madhara ya dawa za kulevya kupata maambukizi ya homa ya ini,Figo,TB,B&C,ukimwi na magonjwa yanayoambukiza kwa njia ya majimaji na damu.



Nae mratibu wa afya ya akili Mkoa Dr Eunice Masango amesema kuwa dawa za kulevya zinaweza kumpeleka MTU kutokuwa sawa kisaikorojia kwa sababu ya matumizi yasiyo sahihi ya dawa hizo  na kuwa na hisia potofu ambazo hupelekea jamii kuzorota kiutendaji na wengine kushindwa kumudu masomo na kuwepo kwa ongezeko la umaskini,uharifu na ubakaji.



Aidha amesema kuwa ushauri nasaha unatumika zaidi katika hatua mbalimbali za tiba,dawa mbalimbali zinazotumika kumpunguzia mtumiaji uteja na usugu pamoja na hospitali mbalimbali za afya ya akili na dawa za kulevya.




Hata hivyo ametaja mikakati iliyopo ni pamoja na  kuanzisha kwa vituo vya Tiba ya methadone ikianza na Manispaa ya jiji la Dar es salaam,Mwanza,Dodoma,Arusha,,Tanga,Mbeya na Zanzibar pamoja na kutungwa kwa Sheria mpya itakayoziba mianya yote iliyopo hivyo itasaidia udhibiti wa tatizo la dawa za kulevya.




Aidha wameitaka jamii kuhakikisha kutowatenga wathirika wa dawa za kulevya kwa kuwapa ushauri juu ya athari za matumizi ya dawa za kulevya pamoja na wao kutojinyanyapaa.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI